Ally Salum Hapi (@AllyHapi) header
Ally Salum Hapi (@AllyHapi) profile picture

Farmer 🇹🇿

Dar es Salaam, Tanzania
Joined March 2013
Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)
Nilisema na leo narudia tena. Ikiwa CHADEMA haitatoka hadharani na kukataa kuendeshwa kwa rimoti na wanaharakati uchwara, utakuwa ndio mwisho wake. Kansa iliyoanza itawamaliza. Lazima wakate kidole. Chama ni taasisi, Chama ni vikao, Chama ni utaratibu.
Kwa maoni yangu, CHADEMA iko katika hali ya “Chama kuwekwa mateka” yaani “party capture”. Watu ambao sio vikao, si viongozi, hawatajwi popote na Katiba yao, wameteka, wanaendesha, kutoa maamuzi & muelekeo wa Chama wakijiita wanaharakati. ANOMIE! Timed bomb!
146
10
21
65
29,998
Kufanya ukatili kwa binadamu kwasababu ya mali au mapenzi ni woga wa maisha. Nyumba zinajengwa, pesa zinatafutwa na wachumba wamejaa tele. Kuanza upya si udhaifu. Wazee wetu hawakuogopa kujipanga upya. Jamii lazima tutafakari kuhusu malezi & afya ya akili.
136
26
17
225
21,168
Nimemtembelea na kutoa pole kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dr. Aman Abeid Karume pamoja na Balozi Ali akarume kufuatia msiba wa Mama yao mpendwa, hayati Bibi Fatma Karume. Mwenyeezi Mungu awajaalie subira na uvumilivu.
9
3
22
2,615
Nimeshiriki maziko ya marhum Mama Fatma Karume Mazizini Unguja. Mwenyeezi Mungu amjaalie maghfira na rehma. Poleni sana familia. Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiuun.
53
4
5
100
13,357
Ally Salum Hapi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026. Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu. Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
65
107
8
354
38,265
Huyu katumwa apeleke rambirambi Kizimkazi kwa Mhe. Rais yeye kakaidi ameenda kulima parachichi. Huku ni kumkosea heshima Mwenyekiti wake TL. Wanaharakati uchwara walio nje ndio wanampa kiburi. Wanamtafutia ya mboga…
194
4
18
95
33,807
Mwanzo Lissu alimuagiza Heche, “endeleeni nisiwakute nilipowaacha, tutagombana…” (waende ktk maridhiano). Juzi ameagiza rambirambi zifikishwe kwa Mhe. Rais Kizimkazi. Ni kipi hamuelewi?!! Picha iko wazi, lakini inahitaji upeo mkubwa kuiona. Siasa ni mbinu…!
192
10
47
91
67,485
CHADEMA imekwama kwenye tope na hawana tena UWEZO na MAARIFA ya SIASA ya kujinasua. Viongozi wake wana MSONGO mkubwa. Wenye nafasi hawana PLAN na wenye IDEA wanahofu kuonekana wasaliti. Wanaharakati FEKI wameshika RIMOTI lakini hawajui kusoma wala kuandika…!
212
5
25
63
148,263
Kwa maoni yangu, CHADEMA iko katika hali ya “Chama kuwekwa mateka” yaani “party capture”. Watu ambao sio vikao, si viongozi, hawatajwi popote na Katiba yao, wameteka, wanaendesha, kutoa maamuzi & muelekeo wa Chama wakijiita wanaharakati. ANOMIE! Timed bomb!
171
20
33
91
35,654
Nimemsikia mara mbili, Tundu Lissu akimtaka Makamu wake Heche kupeleka salamu za pole kwa Mhe. Rais kufuatia msiba wa mwenza wake. Lakini ajabu, hadi sasa sijamuona Heche kufika Kizimkazi ili kupeleka ujumbe huo wa Mwenyekiti wake TL. Liko tatizo kubwa CDM!!
218
13
39
115
144,195
Mhe. VP mteule hongera nyingi kwako Kaka. Mtu wa watu, kijana makini. May God bless you.🇹🇿
13
3
52
3,284
Ally Salum Hapi retweeted
Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri na baraka za Sikukuu ya Maulid. Kumbukizi ya siku hii njema ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) itukumbushe kuendelea kuishi kwa upendo, huruma, uvumilivu na kuwajali wengine. Tusherehekee kwa amani na furaha, huku tukidumisha umoja na mshikamano wetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuibariki nchi yetu, kuitunza katika amani na utulivu, na kutuwezesha kuijenga kwa maendeleo na ustawi wa wote. Mawlid Al Nabi Mubarak.
82
111
6
475
64,662
Met with HE Daniel Francisco Chapo, President of FRELIMO and President of the Republic of Mozambique. I conveyed a message of cooperation and solidarity from HE. Samia Suluhu Hassan, the Chairperson of CCM and President of the United Republic of Tanzania.
1
1
9
2,041
Ally Salum Hapi retweeted
Leo asubuhi nimepata heshima ya kuambatana na Mama yetu, Mama Maria Nyerere, kuelekea nchini Angola ambako pamoja na shughuli nyingine, tutashiriki uzinduzi wa Hospitali ya Rufaa iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hii ni heshima kubwa kwa familia ya Mwalimu Nyerere na Taifa letu kwa ujumla, ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango wake wa kihistoria katika harakati za ukombozi na maendeleo ya Afrika.
43
103
3
392
80,712
Ally Salum Hapi retweeted
Julai 25 kila mwaka ni Siku ya Mashujaa; siku adhimu ya kuwakumbuka na kuwaenzi wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani ya nchi yetu. Kwa ujasiri, uzalendo na kujitolea kwao, walituachia msingi imara wa uhuru, amani, umoja na mshikamano tunaouenzi hadi leo. Tunapowakumbuka mashujaa wetu, tuendelee kulinda tunu walizotuachia kwa kudumisha amani, umoja na kufanya kazi kwa bidii katika kujenga Tanzania yenye maendeleo na ustawi, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mungu Ibariki Tanzania.
65
83
30
212
25,176
Ally Salum Hapi retweeted
Leo nimeungana na viongozi wengine wa Afrika katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya nchini Ghana. Kupitia jukwaa hilo, nimehimiza nchi za Afrika kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kutokomeza UKIMWI, kuboresha huduma za afya ya uzazi na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza. Nimeeleza hatua ambazo Tanzania imechukua kuimarisha sekta ya afya, ikiwemo kuwekeza katika viwanda vya dawa na vifaa tiba, kuongeza bajeti ya afya kila mwaka, kutekeleza programu Bima ya Afya kwa Wote na kuboresha miundombinu ya huduma za afya. Maboresho hayo yanawahakikishia wananchi huduma bora za afya wakati wowote, mahali popote. Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi nyingine na jumuiya za kikanda na kimataifa kuimarisha sekta ya afya na kutafuta suluhisho la pamoja kwa changamoto za afya zinazotukabili.
24
78
2
208
30,034
Ally Salum Hapi retweeted
Shining bright ✨ #FIFAWorldCup
616
9,756
289
73,421
660,444
SPAIN WINS!
248
3,801
57
28,825
221,168
Thank you Spain.
830