Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Z. Homera amefika Mlima Kawetele uliopolomoka Alfajiri ya Leo na Kusababisha Kufukiwa kwa Nyumba 20, Ng'ombe Wanne na Kuharibika kwa Miundombinu ya Shule ya Generation na Mary's katika Mtaa wa Gombe Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
3
1
218
Pia amekiagiza Kitengo Cha Ardhi Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuacha kuwapimia Wananchi Viwanja eneo lenye Changamoto hasa ya Mkondo wa Maji kwa kufanya Kwao hivyo kutasababisha Matatizo kama hayo ambayo yangeweza kuzuilika.
1
148
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Kasim Majaliwa Majaliwa tayari amewasili Mkoani Mbeya na Kupokelewa na Mwenyeji wake Cde: Juma Z. Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya kushiriki Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Leo Tarhe18 March 2024
1
1
118
Zoezi la Utiaji Saini wa Mikataba ya Mfumo MPYA wa Upimaji wa Utendaji Kazi wa Watumishi(PEPMIS) katika Mkoa wa Mbeya limefanyika ambapo limemhusisha Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya Kwenda Kufanya Kazi
ipasavyo katika vituo vyao. Zoezi la Utiaji Saini limefanyika Leo Ijumaa January 05 2023 Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kuhudhuliwa na Washiriki Mbali mbali Wakiwemo Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi na Wataalamu kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Gervas Nyaisonga Leo Tarehe 01/01/2024 amefika Nyumbani kwa Cde Juma Zuberi Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kumtakia Kheri ya Kumbukizi ya Siku yake ya Kuzaliwa
"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea RC Mchapa kazi na sisi kama Kanisa Katoliki tunatambua sana Kazi yako unayoifanya hapa Mkoani kwetu Mbeya Mwenyezi akulinde na akupe Afya Njema ili uendelee kuungoza vyema Mkoa wetu"
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, na Uratibu Mh. Ummy Hamisi Ndereananga amewatembelea Waathirika wa maafa ya kuezuliwa mapaa ya nyumba na kubomoka kutokana na mvua iliyo ambatana na upepo mkali uliojitokeza katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya .
Aidha Katika Ziara hiyo Mh. Ummy Hamisi Ndereananga ametoa msaada wa mabati 500 magodoro 100 saruji 200 Kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliothirika na maafa hayo. Huku akiwasihi kutumia vifaa hivyo Kwa matumizi husika .
1
1
63
Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Comrade Juma Homera amekutana na Kuzungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania Binaya Srikanta Pradhan Ofsini kwake Leo Desemba 09 2023.
RC Homera pia amepata wasaa wa kuongea na Balozi kuhusu mafanikio ya ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye zuru India mwezi Oktoba mwaka huu.



















