Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mtoto wa hayati Edward Moringe Sokoine, Balozi Joseph Edward Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wake wa hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake sasa kimezinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#Sokoine #MaishaYaSokoine #UongoziWaSokoine
Sokoine Foundation retweeted
Replying to @ikulumawasliano
Sokoine Foundation retweeted
SUA tunayo furaha kuwatangazia kwamba kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake” kitazinduliwa 30/9/2024 na Mhe. Dkt. Samia S. Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Sokoine Foundation retweeted
We are pleased to announce that a book on the Late Edward Moringe Sokoine, Former Prime Minister of the United Republic of Tanzania, titled “Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake” will be launched on 30 September 2024 by H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan.
#Sokoine #MaishaYaSokoine #UongoziWaSokoine #TawasifuZaUONGOZI
“Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake”
🗓️ 30 September 2024
Tunayo furaha kuwatangazia kwamba kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiitwacho “Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake” kitazinduliwa tarehe 30 Septemba 2024 na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#Sokoine #MaishaYaSokoine #UongoziWaSokoine #TawasifuZaUONGOZI
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa lbada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Matukio mbalimbali katika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Misa Maalum ya Kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Sokoine Foundation retweeted
Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume aliyehudhuria pia Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Sokoine Foundation retweeted
Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyehudhuria pia Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine.
Sokoine Foundation retweeted
Mapema leo nimeshiriki Misa Maalum ya Kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, iliyofanyika kwenye makazi ya familia yake Monduli, mkoani Arusha. Hayati Sokoine alikuwa kielelezo cha kiongozi mzalendo, mchapakazi, mwajibikaji na mwadilifu kwa umma wa Watanzania.
Tunafanya kumbukizi hizi katika historia ya nchi yetu kwani zinachangia mizizi ya uimara wetu. Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, zinaonesha asilimia 81 ya Watanzania walizaliwa baada ya kifo cha Mheshimiwa Sokoine, hivyo basi Serikali inalo jukumu la kuwashirikisha historia na kumbukizi hizi. Zinatukumbusha wapi tumetoka, wapi tulipo, wapi tunataka kufika na nini tufanye ili kufika, kwa mujibu wa mafunzo ya njia ya waliotutangulia.
Nimeagiza Wizara ya Utumishi kuendelea kutunza kumbukumbu za viongozi wetu hawa na kuhakikisha historia, rekodi na mafunzo ya umahiri wa utumishi wao unafikia jamii, hasa vijana, ili kuwapa mwanga wa kujifunza tumetoka wapi na wapi tunapaswa kwenda kama Taifa katika utumishi wa umma na jamii kwa ujumla.













































