mKigoma ⚓ (@husseinabui) header
mKigoma ⚓ (@husseinabui) profile picture

Muslim.. (Salafy)

sumbawanga
Joined June 2011
Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)Photo by mKigoma ⚓ (@husseinabui)
mKigoma ⚓ retweeted
📌 BAADHI YA BID'A ZINAZOHUSIANA NA MAZISHI 🎓Shaykh Muhammad Nasiruddin Al-Albani رحمه الله ametaja katika kitabu chake *Ahkaam al-Janaa'iz wa Bida'uhaa.. baadhi ya mambo aliyoyahesabu kuwa ni bid'a zinazohusiana na mazishi, yakiwemo.. 1️⃣ Kunyunyizia maji ya waridi juu ya marehemu ndani ya kaburi. 2️⃣ Kutoa sadaka pembezoni mwa kaburi. 3️⃣ Kuweka siku tatu kuwa muda maalumu wa kutoa pole. 4️⃣ Kuzuru makaburi siku ya Idi. 5️⃣ Kusoma Suratul-Fatiha kwa ajili ya wafu. 6️⃣ Kuweka marumaru au mbao juu ya kaburi. 7️⃣ Kuchonga jina la marehemu na tarehe ya kufariki kwake juu ya kaburi. 📚 Kitabu,Ahkaam al-Janaa'iz wa Bida'uhaa cha Shaykh Al-Albaniy رحمه الله, kurasa 317, 319, 320, 325, 329 na 332. Shaykh Al-Albani رحمه الله ametaja katika kitabu hiki zaidi ya bid'a 240 zinazohusiana na mambo ya mazishi. Allah atupe tawfiki ya kuifuata Sunnah ya Mtume Muhammad ﷺ na atuepushe na bid'a katika dini yetu. Allah atujaalie mwisho mwema.
1
3
8
98
mKigoma ⚓ retweeted
Katika Adabu Za Kulazimiana Nazo Siku Ya Ijumaa Kama Leo Ni Hii Ya Kuto Tambuka Watu Na Kukimbilia Safu Za Mbele... #Sunnah #Ijumaa
6
28
430
Kwahiyo @fredkavishe anatudanganya kusema mtaani hakuna kitu?.. Maneno na uhalisia mbona vinapishana?..
KILIMANJARO: Sehemu ya alichokisema Rais Samia Suluhu leo, Novemba 20, 2026, wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026 wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Shule ya Polisi Moshi (CCP). Fuatilia zaidi jamii.app/KujengaImaniPolisi #JamiiForums #Utawala
1
3
272
DARSA: MABADILIKO YA JAMII HUANZIA KWENYE MABADILIKO YA NAFSI ZETU✅ Mada: Athari za madhambi kwa jamii, umuhimu wa Tawhid na kumtegemea Allah katika kutafuta mabadiliko. الحمد لله، والصلاة والسلام على رسول الله ﷺ. Sifa zote njema anastahiki Allah, Mola wa walimwengu. Rehema na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad ﷺ, familia yake na Maswahaba wake. Ndugu zangu katika Uislamu, tunapoangalia hali ya dunia ya leo, tunakutana na matatizo mengi kama ukosefu wa amani, dhuluma, rushwa, migogoro, kuvunjika kwa maadili na kuongezeka kwa maasi. Mara nyingi tunapokutana na matatizo haya, tunaanza kulaumu viongozi, serikali, jamii na watu wanaotuzunguka. Lakini ni mara ngapi tunakaa na kujiuliza kuhusu hali ya nafsi zetu na uhusiano wetu na Allah? Darsa yetu ya leo inatukumbusha kuwa miongoni mwa misingi ya kurekebisha jamii ni kurekebisha imani, matendo na mwenendo wetu. Mabadiliko ya kweli yanahitaji kurejea kwa Allah, kushikamana na Tawhid na kutekeleza wajibu wetu. 1\. Mabadiliko ya jamii huanzia kwenye nafsi za watu wenyewe Allah تعالى anasema: إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ "Kwa hakika, Allah habadilishi hali ya watu mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao." (Surat Ar-Ra'd: 11) Aya hii inatufundisha kwamba mabadiliko ya jamii yanahitaji watu kuanza kujirekebisha wenyewe. Tunataka amani, lakini je, tunaepuka dhuluma? Tunataka viongozi waadilifu, lakini je, sisi ni waadilifu katika majukumu yetu? Tunataka watoto wenye maadili mema, lakini je, tunawalea katika misingi ya dini? Tunataka jamii yenye uaminifu, lakini je, sisi ni waaminifu katika biashara, kazi na mahusiano yetu? Hatuwezi kutarajia jamii ibadilike wakati kila mmoja anakataa kuanza na nafsi yake. Kwa hiyo, Muislamu anatakiwa kuanza kwa kurekebisha imani yake, ibada zake, tabia zake na mahusiano yake na watu wengine. 2\. Madhambi ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ufisadi duniani Allah تعالى anasema: ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ "Ufisadi umeonekana nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyofanywa na mikono ya watu, ili Allah awaonjeshe baadhi ya matokeo ya yale waliyoyatenda, huenda wakarejea katika utiifu." Surat Ar-Rum aya ya 41 Allah anatueleza kuwa matendo mabaya ya wanadamu ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ufisadi duniani. Tunapoangalia jamii zetu, tunakutana na mambo kama kuenea kwa rushwa, dhuluma, uzinzi, kukosekana kwa uaminifu, kuvunjika kwa familia na kula mali za watu kwa njia zisizo halali. Mambo haya yanahitaji kurekebishwa kwa kurejea katika mafundisho ya Allah. Hata hivyo, tunapaswa kuelewa kuwa si kila anayepatwa na janga au mtihani basi ni kwa sababu ya dhambi yake binafsi. Mitihani pia huwapata Manabii na watu wema. Jambo la msingi ni kwamba tunapokutana na matatizo, tusitafute lawama kwa wengine pekee, bali tuanze kwa kujichunguza na kutubia madhambi yetu. 3\. Kuenea kwa maovu ni hatari hata kama wapo watu wema katika jamii Zainab bint Jahsh رضي الله عنها alimuuliza Mtume Muhammad ﷺ: أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ "Je, tutaangamizwa hali ya kuwa wapo watu wema miongoni mwetu?" Mtume ﷺ akajibu: نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ "Ndiyo, pale maovu yatakapozidi na kuenea." (Imepokewa na Al-Bukhari) Hii ni hadith yenye fundisho kubwa sana kwa Waislamu. Inawezekana jamii ikawa na watu wanaoswali, wanaofunga, wanaosoma Qur'an na wanaofanya ibada mbalimbali, lakini maovu yakazidi kuenea katika jamii hiyo. Kwa nini? Kwa sababu kuwepo kwa watu wema pekee hakumaanishi kwamba jamii nzima iko salama ikiwa maovu yanaachwa yaenee bila kupingwa. Uislamu unatufundisha wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu kwa mujibu wa elimu, uwezo na hekima. Allah تعالى anasema: وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ
1
3
7
88
DALILI KUBWA ZA QIYAMAH❗️ Kwa mujibu wa Sunnah sahihi, dalili kubwa za Kiyama ni kumi: * Kutokea kwa Masihi Dajjal. * Kushuka kwa Nabii Isa bin Maryam. * Kutoka kwa Ya’juj na Ma’juj. * Kutokea kwa moshi mkubwa. * Jua kuchomoza upande wa Magharibi. * Kutoka kwa mnyama wa ardhini. * Ardhi kumeza watu upande wa Mashariki. * Ardhi kumeza watu upande wa Magharibi. * Ardhi kumeza watu katika Rasi ya Uarabuni. * Kutokea kwa moto utakaowakusanya watu kuelekea mahali pa mkusanyiko. Rejea: Sahih Muslim, Hadith Na. 2901, kutoka kwa Hudhayfah bin Usayd رضي الله عنه.
1
5
14
201
Barabara ya 17 kwenye chapati na maharage ya kukata ...
Sema Tanga kuna wapishi haswa
1
144
Nimekimbilia kusoma maneno ya mwisho nikidhani utamalizia "HAPPY BIRTHDAY TO ME" 😂😂
13 years later after that terrible fire accident 🙌 Ajali ya moto iliyounguza miguu yangu yote! My Scars, My Strength 💪
4
4
925
🖊📝 DARSA YA FIQH💹 Mada; UTULIVU KATIKA SWALAAH NA MAKOSA YANAYOHARIBU UKAMILIFU WA IBADA✨ AMETUKUKA ALLAH..⏬ Alhamdulillaah, sifa njema zote ni za Allah, Mola wa walimwengu wote. Rehema na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad ﷺ, ahli zake, Maswahaba zake na wote wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Ndugu zangu Waislamu, katika mambo yanayohitaji kupewa umuhimu mkubwa katika ibada ni kutekeleza Swalaah kwa namna sahihi kama alivyotufundisha Mtume Muhammad ﷺ. Watu wengi wanahakikisha kwamba hawakosi Swalaah tano, lakini hawajali sana namna wanavyoitekeleza. Mtu anaweza kuswali kwa haraka, akainama bila kutulia, akainua kichwa kabla viungo vyake havijatulia, na wakati mwingine akawa anaswali huku akili yake ikiwa mbali kabisa na ibada. Hapa ndipo tunapopaswa kujiuliza: Je, tunaswali ili kumaliza jukumu au tunaswali kwa kutekeleza ibada ambayo Allah ametuwekea? Maana ya Twumaaninah na umuhimu wake Twumaaninah ni kutulia katika kila kitendo cha Swalaah bila kukiharakisha. Hii inahusisha kurukuu, kunyanyuka kutoka rukuu, kusujudu na kukaa baina ya sijda mbili. Mtume Muhammad ﷺ alimfundisha mtu aliyekuwa akiswali vibaya kwamba anaporukuu anatakiwa atulie, anapoinuka asimame sawasawa, na anaposujudu atulie katika sijda yake. Hii inatufundisha kwamba Swalaah si mfululizo wa harakati za haraka, bali ni ibada yenye utaratibu, utulivu na unyenyekevu. Hatari ya kuharakisha Swalaah Mtume Muhammad ﷺ aliwahi kumwambia mtu aliyekuwa akiswali bila kutekeleza Swalaah vizuri: «ارجع فصل فإنك لم تصل» “Rudi ukaswali, kwani wewe bado hujaswali. Alimrudisha mara kadhaa mpaka akamfundisha namna sahihi ya kuswali. Hii inatufundisha kwamba kuonekana kwa mtu amefanya rukuu na sijda pekee hakumaanishi kwamba ametekeleza Swalaah ipasavyo. Miongoni mwa makosa yanayopaswa kuepukwa ni kuinuka kutoka rukuu kabla ya kunyooka sawasawa, kufanya sijda kwa haraka na kuinuka bila kutulia. Namna ya kujenga utulivu katika Swalaah...⏬ Muislamu anatakiwa kujifunza sifa sahihi ya Swalaah ya Mtume Muhammad ﷺ na kuitekeleza kwa vitendo. Unapokuwa katika rukuu, tulia mpaka mgongo wako unyooke katika nafasi ya rukuu; unapoinuka, simama sawasawa kabla ya kwenda kusujudu; unapokuwa katika sijda, tulia na usifanye kama mtu anayechuchumaa kwa haraka; na unapokaa baina ya sijda mbili, kaa vizuri kabla ya kusujudu tena. Pia jitahidi kuelewa unachokisoma, kuondoa mawazo yanayokuvuruga na kutambua kwamba umesimama mbele ya Allah. Miongoni mwa du’aa nzuri ni.. ⏬ اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ Allahumma a'inni 'alaa dhikrika wa shukrika wa husni 'ibaadatik. Ee Allah, nisaidie katika kukudhukuru, kukushukuru na kukuabudu kwa namna nzuri. Ndugu zangu, tusiruhusu mazoea yatufanye tusahau thamani ya Swalaah. Huenda mtu akatumia muda mwingi katika shughuli zake za dunia lakini anapofika mbele ya Allah akataka amalize Swalaah kwa dakika chache bila kuzingatia anachokifanya. Tujifunze kuipa Swalaah haki yake, tuwafundishe watoto wetu na familia zetu namna sahihi ya kuswali, na tuwe mifano mizuri kwa wengine. Kumbuka kwamba lengo si kuwa wa kwanza kumaliza Swalaah, bali ni kujitahidi kuitekeleza kwa usahihi, ikhlaasw na khushuu. Tunamuomba Allah azijaalie Swalaah zetu kuwa sababu ya kupata radhi Zake na atuepushe na Swalaah zisizotekelezwa kwa ukamilifu. Aamiyn.
2
1
5
123
Temeke mwisho pale yanafanyika maboresho ya kituo au ndio mambo ya ICD tena.. Walete pesa hizo kata 10 huenda ni kapata mgao ukweni kwangu 😂😂😂..
4
39
2,154
Wasiwasi wangu hizi hekaheka za pale msimbazi zinaweza zikawa ni moja ya PROPAGANDA za mabwana kufanya mitikasi ziende kwa maana kule kwa wakongwe aliyevuwa gwanda kachana mkeka.. Eneweyi jua nikali sana...
9
279
This is the first mosque ever built in Islam: Quba Mosque, in Madinah. On his Hijrah, the Prophet, peace be upon him, came out of the desert mirage and stayed here fourteen nights. He marked it out with his own hand and helped lay its first stones, and his companions finished it. Then he rode on and built the Prophet's Mosque. But every Saturday, walking or riding, he came back here and prayed two rak'ahs. And he said: whoever purifies himself at home, then comes to the Mosque of Quba and prays in it, has a reward like that of an Umrah (Sunan Ibn Majah 1412). Today, a three-kilometre trail, the Quba Walking Trail, runs directly from the Prophet's Mosque to here: walk it, or ride a golf cart. In 2025, over 26 million visitors came, and the mosque is being expanded to ten times its area. Allah says in the Quran: “A mosque founded on righteousness from the first day is more worthy for you to stand in.” (At-Tawbah 9:108, Sahih International) Recitation: Sheikh Abdullah Quraafy Sources: Sahih al-Bukhari 428, 1193, 1194, 3906 · Sahih Muslim 1399 · Sunan Ibn Majah 1412 · Saudi Press Agency · King Fahd Quran Complex · Quran translation: Sahih International Follow @haramain_info for a new film from the Haramain every day. #MasjidQuba #QubaMosque #Madinah #Hijrah #Umrah
6
100
2
450
18,219
DARSA LA TAWHĪD TAWHYID NI MSINGI WA DINI NA SABABU YA KUUMBWA KWETU✅ الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله ﷺ. Ndugu zangu Waislamu! Leo tunazungumzia jambo ambalo ni msingi wa dini yetu, jambo ambalo Mitume wote walitumwa kulifundisha, nalo ni Tawhyid – kumpwekesha Allah katika ibada. Jiulize: Unaweza kuwa na mali, elimu, nyumba na heshima mbele ya watu, lakini je, unamwabudu Allah ipasavyo? Kwa nini Allah alituumba? Allah anasema: وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ Adh-Dhaariyaat: 56 "Na sikuwaumba majini na wanadamu ila waniabudu Mimi." Hivyo, kusudi kuu la maisha yetu si kutafuta mali na mafanikio pekee, bali ni kumwabudu Allah. Tawhyid ina maana gani? Tawhīd ni kumpwekesha Allah katika mambo matatu: * Rububiyyah: Kuamini kuwa Allah ndiye Muumba, Mmiliki na Mruzuku. * Ulūhiyyah: Kuelekeza ibada zote kwa Allah pekee. * Asmaa was-Sifaat: Kuthibitisha majina na sifa za Allah kama zilivyokuja katika Qur'an na Sunnah. Hatari ya shirki...⏬ Allah anasema: إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ An-Nisaa aya ya 48 "Hakika Allah hasamehi kushirikishwa, na husamehe yaliyo chini ya hilo kwa amtakaye." Shirki ni dhambi kubwa sana. Muislamu anatakiwa ajilinde na shirki kubwa na ndogo, ikiwemo kufanya ibada kwa ajili ya kujionyesha kwa watu (Riyaa). Tawhyid inaonekana hata ukiwa peke yako Allah anasema: أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ Al-'Alaq aya ya 14 "Je, hajui kwamba hakika Allah anaona?" Mtu mwenye Tawhyid ya kweli anamwogopa Allah hata akiwa peke yake. Hahitaji kusimamiwa na mwanadamu ili ajiepushe na maasi. Kumtegemea Allah... Allah anasema: وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ At-Talaaq aya ya 3 "Na anayemtegemea Allah, basi Yeye humtosheleza." Tufanye juhudi katika maisha yetu, lakini mioyo yetu imtegemee Allah pekee. Yeye ndiye Mmiliki wa riziki, uhai na kila jambo. Hitimisho...⏬ Ndugu zangu! Siku moja tutaziacha nyumba zetu, mali zetu, magari yetu na vyeo vyetu. Tutabaki na matendo yetu mbele ya Allah. Kwa hiyo, tusijenge maisha yetu tukasahau kusudi la kuumbwa kwetu. Mtume Muhammad ﷺ amesema: مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ Atakayekufa hali ya kuwa anajua kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, ataingia Peponi. 📚Imepokewa na Muslim. Mshike Allah katika raha na shida, katika siri na dhahiri. Hakikisha unaishi katika Tawhyid na unaomba Allah akufishe ukiwa juu ya Tawhid اللَّهُمَّ أَحْيِنَا عَلَى التَّوْحِيدِ، وَأَمِتْنَا عَلَى التَّوْحِيدِ، وَاحْشُرْنَا فِي زُمْرَةِ الْمُوَحِّدِينَ. Ewe Allah! Tuishi katika Tawhīd, tufe katika Tawhīd na utufufue pamoja na watu wa Tawhyid. آمين يا رب العالمين.
3
7
86
Surah Al-Baqarah — (2:285–286)
58
1,713
12
7,073
110,244
How about Kasongo?... Sijamuona wa Malawi...
Wait for the last one 😭😭💀
1
4
264
Alichokifanya huyo mama ni kama vile familia ya Juma Lokole nao walishamkata na hawataki kusikia habari ya aina yoyote kutoka kwake.. Hata watoto aliozaa hawakanyagi kwa ndugu zake wala kwa bibi yao upande wa kiume.. Na mwanamke alipojua akavunja ndoa..
Ushuhuda huuu unaanza mnamo mwaka 2018🥱..ilikuwa alfajiri iliyopoa ilikuwa sio Alfajiri ya kawaida,nilipokea cm kutoka kwa Udugu wangu Vumilia aliyeko morogoro wakati huo me niko Dar hapo maeneo ya gongo la mboto mzambarauni mashineni kwa mama Dickson🥱 Da vumi (tulizoea kumuit
4
29
6,720
Game 11 kashinda 1 sare 3 vipigo 7.. Hamnakocha na pia hatuna wachezaji..
1
1
4
959
Hata msikitini spika iwe kwa ajili ya dhana tu baada ya hapo watumie spika za ndani..
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema hataki kuona nyumba za ibada zikijengwa au kuanzishwa kila mahali bila utaratibu maalumu, akieleza kuwa hali hiyo inaweza kusababisha kelele na usumbufu kwa wakazi.
2
199
Kama msomi wa mambo ya kodi kaswindwa kujibu hili swali mie ndio nitaelewa kweli.. 😂
1
1
4
293
Mwembe chai ikawaje?...
Sheikh Khalifa Khamis dhidi ya Augustine Mrema mwaka 1995. Nchi inetoka mbali hii😃.
1
144