NHIF Tanzania (@nhiftz) header
NHIF Tanzania (@nhiftz) profile picture

The Official Account of the National Health Insurance Fund (NHIF) of Tanzania I Ukurasa Rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Customer Service: 199

Dodoma, Tanzania
Joined October 2015
Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)Photo by NHIF Tanzania (@nhiftz)
NHIF Tanzania retweeted
Alhamisi hii kwenye Afya Asubuhi tutakuwa live na Meneja kutoka NHIF Mkoa wa Mwanza, Jarlath Mushashu. Ungana nasi kuanzia saa 7am - 10Am . Cc: @nhiftz ... Tusikilize kupitia 96.9Mhz || Online: afyaradio.co.tz .................. Tufuatilie: @afyafm . . #afyaradio
1
2
344
BIMA YA AFYA SULUHISHO LA HUDUMA BORA ZA AFYA Na Majid Abdulkarim, KATAVI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kujiunga na huduma ya Bima ya afya kwa wote ili kuzidi kuimarisha huduma za Afya nchini Pia Mhe. Rais amewataka wananchi wa Katavi kuuza mazao ili waweze kupata fedha na kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote. Kauli hiyo ameitoa leo Julai 13, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Serikali wakati wa kilele cha wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi kilichohitimishwa mkoani Katavi Dkt Samia amesema Serikali imeendelea kuweka misingi madhubiti ya vyanzo vya uhakika vya fedha ili kutekeleza bima ya afya kwa wote. Amesema gharama za matibabu kwa sasa zimekuwa juu na suluhisho ni bima ya afya kwa wote. "Niwaombe sana ndugu zangu wa Katavi unajua wakati mwingine umaskini ukiukumbatia na wenyewe unakukumbatia mnapouza mazao jitahidini kuhakikisha mnajiunga na bima ya afya kwa wote uweze unatibiwa mwaka mzima bila usumbufu" amesema Mhe. Rais na kuongeza "Tukifanya hivyo watanzania wote tutapata fursa ya kupata matibabu mazuri na ya viwango kulingana na uwekezaji mkubwa ulofanywanaSerikali yenu,"amesisitiza Dkt Samia.
11
8
1
38
10,379
BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA AFYA KWA KISHINDO Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha kwa kishindo Bajeti ya Wizara ya Afya ya jumla ya Shilingi Shilingi trilioni moja, bilioni mia tatu kumi na moja, milioni mia nane thelathini na saba, laki nne na sitina na sita elfu (1,311,837,466,000.00) ili kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa Mwaka wa Fedha 2024 /2025. #TunaboreshaAfya โ€“ at Dodoma, Tanzania
1
6
19
2,025
NHIF Tanzania retweeted
Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kupitisha kwa asilimia 100 Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2024/25. Nawashukuru kwa Pongezi nyingi mlizotupatia. Tuna deni kubwa sana kwenu, tuna deni kubwa kwa Watanzania, tuna deni kubwa kwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan la kujituma zaidi ili kuboresha Huduma za Afya. Pamoja na mafanikio mengi na makubwa tuliyoyapata bado sekta ya afya nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Tutaendelea kujituma ili kuzitatua. Nawashukuru kwa maoni na ushauri wenu mliotupatia. Tutazingatia maoni na ushauri wenu #KaziIendelee ------- Posted @withregram โ€ข @jambo_online_tv Bunge la Tanzania limeridhia kwa asilimia mia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni moja, bilioni mia tatu kumi na moja, milioni mia nane thelathini na saba, laki nne na sitina na sita elfu ili kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa Mwaka wa Fedha 2024 /2025. Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa, kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa na kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini pamoja na kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
59
27
8
197
31,992
ORODHA YA DAWA 178 ZILIZOJUMUISHWA KATIKA KITITA KWA KUZINGATIA NGUVU, MUUNDO NA MUUNGANIKO. Pongezi kwa Kamati ya Kitaifa ya Tiba na Dawa kwa kutoa nyongeza ya tafsiri sahihi ya Muongozo wa Tiba kuhusu ujumuishwaji wa nguvu, muundo na muunganiko wa dawa zinazotajwa katika orodha ya taifa ya dawa muhimu. #TunaboreshaAfya #MtuniAfya
33
59
11
196
36,401
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya @nhiftz umeendelea kufanya jitihada za kupunguza harasa ambapo katika mwaka wa fedha 2022/23 NHIF ilipata hasara ya Shilingi Bilioni 156.77 ikipungua kutoka Shilingi Bilioni 205 ya mwaka 2021/22. CAG amesema moja ya mambo yanayoupa mzigo mkubwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni wastaafu na wenza wao kupata huduma bila kuchangia ambapo kwa mwaka huugharimu mfuko shilingi Bilioni 84.7 Charles Kichere amepongeza juhudi zinazofanywa na NHIF katika kuongeza wananchama wapya ambapo imefanikiwa kuongeza wanachama wapya kwa asilimia 14.6. Changamoto nyingine ni kuongezeka kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanaugharimu mfuko shilingi Bilioni 130.8 kwa mwaka, na hivyo kuhatarisha uhimilivu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Kuhusu deni la Shilingi Bilioni 208 ambalo NHIF inaidai Serikali, CAG amesema kuwa Serikali imepanga kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 180 katika mwaka wa fedha 2024/25 kupunguza deni hilo.
8
8
1
38
4,044
NHIF Tanzania retweeted
(โœ๐Ÿป na wachambuzi wetu wa mambo ya afya) WATAALAMU WA AFYA NI VYEMA TUWE WAKWELI KULIKO KUPOTOSHA HILI LA MADAWA KUFUTWA!! WAKATI kuna sintofahamu na mkanganyiko ambao sasa unatafutiwa ufumbuzi ni vyema watu wenye uelewa wa mambo haya mkatumia taaluma zenu kuelewesha watanzania juu ya jambo hili kuliko kuwa sehemu ya kuleta vurugu na mikanganyiko. Lazima tufike mahali tujue kuwa watanzania hawasomi haya mambo na hawana huo muda wao wakikutana na mambo humu mitandaoni basi ndiyo agenda yaani. Sisi Kigogo Media kwa kuwa tunafuatilia jambo hili kwa ukaribu sana na kwa kuwa lina maslahi makubwa sana kwa watanzania tumejipa muda kusoma na kuhoji watu wenye taaluma hii na haya ndiyo majibu yao na tungependa tuanzie hapa kwa hoja hizi kuliko kuleta taharuki. Nitaanza kwa mfano mdogo sana, HIVI DAKTARI AKIKUANDIKIA PANADOL LAKINI UKAENDA DUKA LA MADAWA WAKAKUAMBIA KUWA PANADOL HAKUNA KUNA PARACETAMOL hii tunaita kuwa dawa imefutwa au haipo? Kama jibu ni HAPANA basi tulia hapa tufafanue jambo hili kwa ufasaha! Katika kutafiti jambo hili tumefahamu kuwa huduma za afya nchini hutolewa kwa kuzingatia muongozo wa Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines Lists โ€“ STG/NEMLIT. Mwongozo huu unabainisha magonjwa yote pamoja na dawa zinatotakiwa kutibu magonjwa hayo. Tumesoma jinsi ambavyo muongozo huu unaandaliwa na tumegundua kuwa wafamasia,kamati ya tiba ya taifa (NMTC) na mganga mkuu wa serikali ni wahusika wakuu kwenye mchakato huu. Tumebaini kuwa muongozo huu sasa ndiyo hutumiwa na madaktari kuandikia wagonjwa madawa kutokana na aina ya ugonjwa na ngazi ya kituo cha kutolea huduma za afya kuanzia zahanati,vituo vya afya,hospitali za wilaya,hospitali za mikoa hospitali za kanda na mwisho kabisa hospitali za taifa. Tumejulishwa na kusoma huu muongozo na kugundua kuwa ndiyo hutoa orodha ya dawa zitakazokuwa zinaandikwa na madaktari, kutolewa na wafamasia, kununuliwa na MSD na pia kugharamiwa na NHIF kupitia vitita vyao kwa mujibu wa Sheria. Kwa hiyo MSD wananunua na kuagiza dawa kwa ajili ya matumizi nchini kwa kuzingatia muongozo huu. Sasa kama hivi ndivyo NONGWA ipo wapi? Sisi tulijizuia sana kuchangia jambo hili kwa sababu ni la kitaalamu sana na lilihitaji tulisome na kulitafiti kwanza kabla ya kujiingiza kwenye mijadala ambayo kwa kiasi kikubwa sana tumerushusu watu wasio na taaluma wala kujua mambo haya ndiyo wanatoa kauli za kitaalamu hasa eneo hili nyeti sana la madawa. Kwenye mahojiano yetuna wahusika juu ya jambo hili tumeelezwa kuwa sababu za jumla za mabadiliko ya dawa kwenye Mwongozo wa Matibabu (STG/NEMLIT) ni kama ifuatavyo; 1. Ujio wa dawa mpya na zilizo bora zaidi kuliko zilizokuwa zimebainishwa mwaka 2016, hivyo mapitio ya STG/NEMLIT ya mwaka 2021 yalizingatia uwepo wa dawa bora zaidi sokoni; 2. Usajili na upatikanaji wa dawa husika katika soko la Tanzania pamoja na gharama zake kwa mwananchi kuweza kununua akiandikiwa na daktari; 3. Dawa nyingi zilizo katika muunganiko (Fixed Dose Combination โ€“ FDC) zinakuwa na majina ya kibiashara, kuepuka hili Mwongozo unazitaja dawa hizo moja moja na siyo katika muunganiko (FDC); 4. Pia dawa moja inaweza kuwa na muundo (formulation) zaidi ya mmoja (mfano syrup, Injection, tablet, suspension, capsule n.k) kwa kuzingatia kuwa muundo unabadilika kwa haraka, Mwongozo unatambua na kuidhinisha matumizi ya dawa (molecule) kwa jina halisi (generic name). Vivyo hivyo kwenye nguvu (strength) dawa moja inaweza kuja kwa nguvu au ujazo tofauti mfano 1mg, 2mg, 5mg, 7mg na 10mg Mwongozo unatambua matumizi ya dawa (Molecule) husika kwa ugonjwa husika. Kutajwa kwa formulation mojawapo au strength mojawapo hakuondoi matumizi ya nyingine zilizobaki maana uhitaji wake unategemea na umri, uzito, hali ya mwili, hali ya ugonjwa n.k SABABU kubwa sana nay a msingi ya kuondolewa kwa baadhi ya dawa ni kuingizwa zingine zilizoonekana kuwa ni bora zaidi au zinapatikana kwa urahisi au zina maudhi/madhara kidogo. Mifano michache ya uamuzi huu ni hivi: Aceclofenac imeondolewa na kuletwa Diclofenac Amoxycillin oral liquid imeondolewa na kuletwa vidonge vya amoxycilli myeyuko ambavyo vinamuepusha mtoto na sukari ya kwenye syrup pia utunzaji ambapo wengi hawa friji za kutunzia hasa vijijini. Alendronic acid tabs imeindolewa na kuletwa Ibandronate ambayo ni bora zaidi na inatoweka haraka (masaa 37 โ€“ 157) katika mwili wa binadamu wakati Alendronic ni takriban miaka 10 Artesunate & Metakelfin tabs imeondolewa kutokana na madhara ya Metakelfin na kuletwa Alu Tumepitia listi nzima ya madawa 176 yanayolalamikiwa kuwa yameondolewa lakini kiuhalisia ni kuwa madawa yote yamepewa mbadala na hivyo ndivyo muongozo unavyotakiwa kufuata na watoa huduma na NHIF wamekubaliana nao hivyo na tungependa sasa wanataaluma muweke hili jambo sawa na kitaalamu ili kuondoa huu mkanganyiko ambao kila mtu sasa kawa mfamasia na kutoa maelezo ya nini kinaendelea. Watu wetu hawasomi haya mambo na wanachofanya nikukokota mambo wanayokutana nayo mitandaoni na kuyafanya ndiyo uhalisia. NHIF wakati mnabandana na mambo ya vitita na watoa huduma wa afya matukio haya yanatosha kuonyesha kuwa idara ya elimu kwa jamii au wanachama wenu wana kazi kubwa sana ya kufanya ili kuelewesha umma juu ya mambo haya na jinsi yalivyo. Kwa sababu kama tuna muongozo wa dawa gani zitumike na kwa magonjwa gani na mnazi update kila baada ya muda sasa ugumu uko wapi kwa watu kuelewa? NI kweli madawa haya 176 yameondolewa lakini yameondolewa na kuna mbadala bora zaidi kwa kuzingatia vigezo vya kimatibabu na kufamasia. Siyo kwamba yameondolewa na sasa watu wanaambiwa wanatumia mizizi kujitibu UTI au malaria,hapana kinachotokea hapa ni watoa huduma hawataki kununua dawa kule MSD kama ambavyo muongozo unasema halafu wanatoa kauli ya jumla tu kuwa madawa 176 yameondolewa! Kwa nini hawasemi yameondolewa kwa kuwa kuna mbadala bora na zinazotibu lwa ufanisi zaidi? HITIMISHO la utafiti wetu ni kuwa mwongozo wa matibabu na orodha ya dawa muhimu nchini huzingatia magonjwa yote yanayofahamika na yanayowakabili watanzania, hivyo hakuna ugonjwa ulioachwa bila dawa kwa mujibu wa muongozo huu ambao tumeusoma na kuchambua kwa zaidi ya siku 4. Vilevile ni muhimu kuelewa kuwa teknolojia ya dawa inabadilika kwa kasi sana na gharama za matibabu ni kubwa sana hivyo ni lazima kuwa na mwongozo wa matibabu ili kuhakikisha taratibu za matibabu zinafuatwa kwa matokeo bora. Mfano ni miaka ile ya 1990 ulikuwa ukiumwa kikohozi unakwenda na chupa yayo hospital na kupewa dawa inaitwa "mokje wa punda" je? dawa ile ipo mpaka leo? Haipo kwa sababu kuna dawa bora zaidi na maendeleo ya teknolojia yamesaidia hilo sana. ANGALIZO MUHIMU SANA Mabadiliko kwenye matibabu yasipo dhibitiwa yanaathari kubwa kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Hivyo, kitita cha NHIF na nyie watoa huduma wa afya ni muhimu sana kuzingatia mabadiliko haya, aidha kwa maeneo yaliyoonesha upungufu kaeni na kuzungumza na kuhakikisha kitita hakitofautiani na mwongozo wa matibabu wa mwaka 2021 ili msitusumbue na kuhangaisha wananchi na mambo haya! #KigogoMediaUpdates
3
75
5
1,002
156,885
NHIF Tanzania retweeted
UFAFANUZI WA MWONGOZO WA DAWA NCHINI NA KUONDOLEWA BAADHI YA DAWA KATIKA KITITA CHA NHIF @ummymwalimu @wizara_afyatz @TZMsemajiMkuu @bima_afyatz #nhiftz #nhif #bima #bimayaafyakwawote
11
10
1
31
5,298
Mkurugenzi wa Huduma za Dawa na Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi amefafanua juu ya baadhi ya dawa kuondolewa katika Muongozo wa matibabu ili kupisha dawa bora zaidi zinazoendana na wakati wa sasa kwa magonjwa yote yanayowakumba watanzania na pia kuepuka uandishi wa dawa zenye muunganiko yaani Fixed Dose Combonation kwa kuwa nyingi zinakuwa zimebeba majina ya kibiashara. Ameisisitiza kuwa mwongozo huo umezingatia upatikanaji wa dawa zote muhimu kwa magonjwa yote nchini na kwa ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.
9
11
24
3,437
"Kitika kipya cha mafao ya NHIF kupunguza mfumuko wa gharama za matibabu nchini" Naibu Waziri wa Afya @dr_mollel
16
9
3
44
52,303
NHIF Tanzania retweeted
Asanteni Bochi Hospitali na Wote waliorudisha huduma kwa wanachama wa NHIF. Tunawashukuru sana sana. Ninawaahidi kuwa tutafanya maboresho ktk maeneo mahususi mtakayoyaainisha ndani ya muda mfupi. #MaishaYaWatuKwanza โ€“ at Dar es Salaam, Tanzania
171
61
38
650
126,682
"Wizara iliamua kusitisha kitita kipya cha NHIF cha mwaka 2023 na kuunda kamati ya serikalini, sekta binafsi na Taasisi za Bima kwa ajili ya kuishauri serikali, wakakutana wakasikiliza hoja za NHIF, wakasikiliza hoja za Hospitali binafsi, walifanya vikao vingi, na nimesikitishwa tunao ushahidi wa maandishi, barua walizopelekewa na minutes walizokaa kwenye hivyo vikao, baada ya kuitwa kamati ile ikaenda mpaka ndani, ikaja na vigezo kuhusu maboresho ya kitita ambacho NHIF wameleta pamoja na Hospitali binafsi yameletwa bila kuathiri upande wowote" -Waziri Ummy
2
7
13
5,810
"Kama mtu anafanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni kamati ikapiga mahesabu, vinatumika vifaa gani na vitagharimu hivi lakini na vitenganishi vinavyohitajika, atakuwepo Daktari, atakuwepo Muuguzi, atakuwepi Mfamasia, atakuwepo mtu wa usingizi, atakuwepo mtu wa Maabara, kamati imeweka vigezo, watuletee vigezo. Kamati ya Dkt. Sakwale imeenda mbali ikaweka ikasema tunaweka uchakavu wa vifaa vinavyotumika, wakaongeza kigezo cha tano gharama za uendeshaji, kigezo cha sita wastani wa faida, ndugu zangu nawaomba warudi kwenye meza ya majadiliano kamati ya Dkt. Sakwale imeweka vigezo walete vigezo vyao, waseme vigezo hivi havipaswi kutumika katika kukokotoa gharama au bei za huduma za afya" -Waziri Ummy
27
13
5
82
22,792
"Fedha atakayelipwa Daktari Bingwa aliyepo hapa Sokoine Lindi (Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi) hakuna ubaguzi, fedha atakayolipwa Daktari Bingwa wa Muhimbili ndio atalipwa Daktari Bingwa wa Katavi, Daktari Bingwa wa Rukwa, Daktari Bingwa wa Kigoma nk, fedha atakayelipwa Daktari wa kawaida aliyeko Dar es Salaam ndio atakayeliowa Daktari aliyepo Mnazi mmoja atalipwa sawa, lengo la kitita hiki pia ni kuvutia Madaktari Bingwa na wataalamu wengine kufanya kazi" -Waziri Ummy
14
6
43
10,649
"Lakini hili wakati wanalikubali, haya mengine wanasema wanayakataa watuambie kwa vigezo gani, turudi kwenye meza ya majadiliano, kwa hiyo serikali imeeleza NHIF kuendelea na kitita kipya lakini wazingatie maoni na mapendekezo ya kamati ndio maana hata sasa bei za kumuona Daktari NHIF ikabidi abadilishe arudie kama kamati ilivyoshauri" -Waziri Ummy
4
5
2,516
"Napenda kuwashukuru sana vituo/Hospitali binafsi na Vituo vilivyo chini ya Taasisi za dini ambavyo vimeendelea kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF hadi sasa. Hakika wameonyesha utu, uzalendo na dhamira ya wazi ya kushirikiana na Serikali yao katika kutatua changamoto zilizopo pasipo kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi" @ummymwalimu
8
6
2
24
3,646
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akitoa ufafanuzi juu ya utoaji huduma za Mfuko huo katika Hospitali binafsi kufuatia kitita kipya cha mafao kinatarajiwa kuanza kutumika Machi 1, 2024. #MtuniAfya @nhiftz
10
18
3
53
6,837
NHIF Tanzania retweeted
Kesho tar 1 Machi 2024 nitatoa kauli ya Wizara kuhusu suala hili. Wote tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya @nhiftz unaendelea kuwa himilivu, endelevu na stahamilivu kwa maslahi ya pande zote - yaani Wananchi, wamiliki wa vituo vya kutolea huduma za afya, NHIF na sekta ya Afya kwa ujumla. โ€“ at Lindi, Tanzania
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MABORESHO YA KITITA CHA MAFAO KWA WANUFAIKA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA @nhiftz
122
33
23
175
63,726