Voice of Bongo (@voiceofbongo) header
Voice of Bongo (@voiceofbongo) profile picture

Welcome to the Official VOB Twitter Page. (Disclaimer: The views expressed here do not necessarily reflect the views of Voice of Bongo

Tanzania
Joined July 2015
Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)
Kijana Kefasi Mtega mwenye umri wa miaka 30 anayetuhumiwa kuhusika na wizi wa miundombinu ya umeme Iganjo hadi Sumbawanga, ameomba Viongozi wamuhoji kwa Lugha ya Kiingereza pekee kwani ndiyo lugha anayoielewa pekee.
2
369
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amezitaka Jumuiya za kiraia nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha umoja, mshikamano na kulinda amani. Wito huo ameutoa wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 70 ya Usajili wa
1
291
Jumuiya za Kiraia katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. Katambi amesisitiza kuwa,Taifa letu lina historia nzuri katika kulinda amani na utulivu wa nchi, hivyo ni vizuri kuendelea kuilinda historia hiyo
1
107
Tume ya Rais ya kuchunguza vurugu na uvunjifu wa amani uliotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa oktoba 29 2025 sasa ipo katika wilaya ya Temeke. Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Shaaban Lila amewataka wananchi wa wilaya ya temeke kufika katika chuo kikuu kishiriki
2
322
cha elimu DUCE ili kutoa ushahidi kwa wanayoyajua kuhusu kilichotokea wakati wa vurugu hizo. Kwa upande mwingine, Jaji Shaaban Lila amewahakikishia wananchi wanaokuja kutoa ushahidi kuhusu usalama wao na usiri wa watakayoyasema katika tume hiyo.
61
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kimkakati katika kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha.
1
247
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya ulinzi wa njia ya treni ya mwendokasi (SGR) pamoja na ukarabati na ujenzi wa mitaro ili kuzuia mafuriko katika makorongo yaliyoonesha kupelekea kuathiri makazi ya wananchi.
1
73
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amewasili mkoani Tabora leo, Septemba 26, 2026, kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu inayotekelezwa na Sekta ya Ujenzi mkoani humo.
1
375
Akiwa mkoani Tabora, Waziri Ulega atakagua miradi mbalimbali ya barabara na miundombinu mingine inayotekelezwa katika mkoa huo, ili kujionea maendeleo ya miradi hiyo, pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake.
1
58
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawakumbusha wananchi kuchukua tahadhari ya matumizi salama ya umeme wakati wa mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. Ukiona hitilafu ya umeme, toa taarifa kwa kupiga namba 180, kupitia mitandao yetu ya
1
291
kijamii au makundi rasmi ya TANESCO ya _WhatsApp_ yaliyopo kote nchini. Umeme Salama, Usisubiri Athari, Chukua Tahadhari.
93
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Mark Kihulla, amekutana na Waandishi wa Habari kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2026/2027, akisisitiza
1
213
umuhimu wa uhakiki wa mita za maji katika kuhakikisha usahihi wa vipimo na kulinda maslahi ya wananchi. Katika utekelezaji wa majukumu hayo, WMA imeendelea kuhakiki mita za maji, zikiwemo mita mpya na zile ambazo tayari zinatumika katika makazi ya wananchi. Kwa mwaka wa
1
73
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Mark Kihulla, ameeleza hatua zinazochukuliwa na Wakala katika kusimamia usahihi wa vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya
1
196
WMA kwa mwaka 2025/2026 na mwelekeo wa mwaka 2026/2027, amesema Wakala huzingatia sheria za kitaifa pamoja na matakwa ya kikanda na kimataifa katika kuhakikisha vipimo vinakuwa sahihi na vinaaminika.
27
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umejenga miundombinu ya kisasa ya uzalishaji wa chumvi kwa wanawake wa Kijiji cha Nsunsu, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, hatua inayotarajiwa kuongeza tija, kuboresha ubora wa chumvi na kuongeza kipato.
1
240
Miundombinu hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko katika uzalishaji ambao kwa muda mrefu umekuwa ukifanyika kwa kutumia mbinu za jadi, kupunguza muda wa uzalishaji na kuongeza kiwango cha chumvi inayozalishwa.
68
Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst) Hamis Rajab Semfuko leo Septemba 10, 2026 ametembelea hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kujengwa katika eneo hilo, Mkoani Arusha.
1
329
Leo jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Marianne Young amekutana na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu sekta ya madini nchini Tanzania na fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania.
1
300
Mkutano huo ulijadili kuhusu uwekezaji, uongezaji wa thamani, na kuhakikisha sekta hiyo inachangia katika ukuaji wa uchumi unaoshirikisha wote. Tanzania na Uingereza zitaendelea kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili ili kudumisha ustawi wa mataifa hayo.
46
Mwenyekiti wa Zamani wa klabu ya Simba na Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage amesema tayari ametoa ushahidi wake kwenye tume ya Jaji Lila na amewataka wakazi wa Ilala kujitokeza katika viwanja vya karimjee ili kutoa ushahidi kwa
1
395
wanayoyafahamu kuhusu ghasia za uchaguzi wa october 29 mwaka 2025.
33
Tume ya Uchunguzi wa ghasia za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 inayoongozwa na Jaji Lila imeanza kusikiliza ushahidi kwa Wananchi wa Wilaya ya Ilala kuanzia leo Jumatatu August 31 hadi Septemba 4, 2026 katika viwanja vya Karimjee Posta, Wananchi wote wanakaribishwa.
288
"Nitoe rai kwa Watanzania wote kuwa na tahadhari na jambo hili [mvua za El Nino] ambalo tayari tumekwisha kutahadharishwa [...] Tuendelee kuchukua tahadhari ili maafa yasitokee." - Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu
1
1
235
"Pasiwepo na kushusha abiria nje ya stendi wala kupakia abiria nje ya stendi. Wale wa kupanda wapandie stendi na wale wa kushushwa washushiwe stendi." - Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu
348
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amempongeza Waziri wa zamani wa Nishati, Deogratius Ndejembi, baada ya kupendekezwa na vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2
1
2
872
Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo leo Alhamisi, Agosti 27, 2026, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.
27
Watanzania 173 waliokuwa wakiishi katika Jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, wamewasili nchini baada ya kuamua kurejea nyumbani kwa hiari kufuatia vuguvugu la kupinga wageni linaloendelea nchini humo.
1
1
216
Zoezi la kuwarejesha raia hao limefanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Afrika Kusini, ambapo Serikali ya Tanzania imetoa ndege maalum kwa ajili ya kuwawezesha raia hao kurejea nchini.
50