
Database analyst , IT advisory, Database Developer, Payroll System developer, HR&bio-metric system expert, #ManUnitedfan.
Joined February 2020
- Tweets3.3K
- Following1.9K
- Followers1.6K
- Likes10.8K
BestHope retweeted
Mtoe Lissu, Mlipe Stahiki Zake Zote.
Itisha kikao cha Maridhiano ya Kitaifa. Badilisha Katiba. 2029-2030 twende kwenye Chaguzi Huru na Haki.
Asante.
A letter to you, 🙏
Wale wajinga waliokataa starlink kwa kigezo cha ujasusi watembelee website hii waone kama kuna tunachoficha. Tembelea weka eneo ulipo uone satellite ngapi zimepita eneo hilo na picha zilizopigwa.
watched.earth/
1
314
BestHope retweeted
Lazarus was dead for four days before Jesus showed up. Sometimes God waits until it looks impossible so nobody can take credit for the miracle🥹
BestHope retweeted
Yaani huyu hakimu na mawakili wa CCM hawana akili. Wameshindwa hata kujifunza kupitia hata hizi clip mbona wameaibka sana. Wamejivua nguo makalio yako wazi
BestHope retweeted
“Today the High Court has confirmed what we have said from day one: the treason charge was a political fabrication. The prosecution failed to prove any intention to intimidate the government.
Instead of ordering my release after 577 days in detention, the court has convicted me of an offence I was never charged with and never given a chance to defend.
This is not justice. This is damage control.
History will record how the court searched for a lesser charge simply to keep me in prison.” Tundu Antipas Lissu
November 6, 2027
—Admin.
BestHope retweeted
“If you feel pain, you are alive.
If you feel other people's pain, you are a human being.”
—Leo Tolstoy
Kwa hukumu iliyotolewa pasipo na option ya faini ni wazi kwamba waliosimamia mpango mzima wa kesii hii hawana nia njema na hawajawahi kuwa na nia njema na mweshimiwa. Wana nia katili ni vile tuu wameshindwa kuitekeleza na kushindwa huko wameona wamkomeshe kwa hukumu ya miaka 4.
261
BestHope retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 6, 2026
Last time tuliishia part 493 so leo tunaendelea na -;
Part 494.
Karani amewasha kipaza sauti kutoa Tangazo kuwa watu wakae kwenye viti vyao na simu zao wahakikishe zinatolewa sauti na milio ya aina yote.
Waandishi wa Habari na wao wako wakutosha sijawahi kuwaona Mahakamani kwenye kesi yoyote wakiwa wa idadi hii ni wengi sana sana.
Hata waandishi ambao huwa hawajagi kabisa naona wamekuja, namuona yule Charles William wa Wasafi nae leo yupo kuna mtiti hapa unataka kutokea, wanataka kumnyayua Mzee Mpoki alienda kukaa viti vya Mawakili wa Serikali 😂😂😂
Wale watoto wa serikali ambao huwa wanakaa kwenye benchi la nyuma ya akina Katuga, leo wamekaa mawakili wa Mhe. wabishi hatari wamegoma kusimama.
Ameingia Mheshimiwa Lissu akiwa na vibe na kusema TUTAFIKA! TUTAFIKA! TUTAFIKA!
Wameingia Mawakili wa Serikali.
MAJAJI walikwisha ingia hata kabla Mawakili wa Serikali hawajaingia.
Muda huu wanawasha zile mic zao ili tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema karani tuendeleeee.
Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasoma namba ya shauri karani.
Anasimama Katuga anajitambulisha niko na wenzangu Job Mrema, Cathbert mbiringe ba Winniwa Kasala
Tunaiwakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri linakuja kwa ajili ya uamuzi na upande wa Jamhuri tuko tayari.
Mshitakiwa vipi wewe?
Mheshimiwa Lissu anasema niko tayari pia.
Majaji Wanateta pale kabla hawajaanza kuusoma huo uamuzi.
Jaji Ndunguru anasoma, naomba tusikilize Hukumu.
Katika shauri hili Mshitakiwa Tundu Lissu anashitakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)d kanuni ya Adhabu 2023.
Maelezo yanasema kwamba Tarehe 03/04/2025 Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam mshitakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Kudhihirisha nia hiyo kwa kitendo cha kutamka maneno ya wanasema kitu kimoja sahihi kwamba msimamo huu unaashiria uasi na tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kuleta mabadiliko na huu uchaguzi tutauvuruga.
Mshitakiwa alikana hati ya mashitaka na shauri likaanza kusikilizwa.
Kama ilivyo kawaida upande wa Mashitaka waliongozwa na Wakili Renatus Mkude na Ajuaye Zengeli na Nasoro Katuga na anawataja Mawakili wote wa Serikali.
Upande wa Mashitaka walileta mashahidi 17 na ambao kati yao 17 walikuwa ni mashahidi wanaolindwa.
Na mshitakiwa alijiwakilisha Mwenyewe na alileta Mashahidi wanne na yeye alikuwa watano na pia utetezi walitoa vielelezo anbavyo ni 16.
Baada ya upande wa mashitaka kutoa ushahidi na mshitakiwa alijitetea na walileta hoja za majumuisho walileta hoja hizo.
Mahakama hii iliongozwa na kanuni mbalimbali ni
1. Katika Mashauri ya Jinai mwenye jukumu la kuthibitisha ni Upande wa Mashitaka.
2. Kutiwa hatiani kwa mshitakiwa hakutazingatia udhaifu wa mshitakiwa.
3. Ushahidi utatazamwa kwa ujumla wake na sio vipande.
4. Mashaka yoyote hata kama yana uzito kiasi gani hayabadilishi burden ya kuthibitisha shitaka.
Mahakama hii imechunguza kwa umakini hati ya mashtaka, ushahidi na mawasilisho ya pande zote mbili na kuja viini vitatu vya kuthibitisha
Moja: Iwapo Mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT
Mbili: Iwapo Mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali.
Tatu: Iwapo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kusambaza maneno hayo.
Mahakama imeona ni vyema ifafanue kwanza katika hoja ambazo zinaonekana kama mapingamizi wakati wa hoja za majumuisho ya mshtakiwa.
Kwa kuwa hati ya mashtaka ndio inayoanzisha shauri la jinai ni vyema tuamue kwanza kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka. Mshtakiwa alisema hati ya mashtaka ina mapungufu katika maeneo matatu moja kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kinazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu, pili hati ya mashtaka haikutoa taarifa muhimu ambazo zilipelekea ashindwe kutoa utetezi kamili na tatu hakuna lengo lilioonyeshwa katika hati ya mashtaka.
Part 495 itaendele kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Dear @ManUtd , Follow this professional advice to lift your curse. Obey and you shall be unstoppable.
Never play these players at the same time, regardless of their position:
- Yoro and Heaven
- Cunha, Mbeumo and Rashford (any 2)
- Baleba and Maino.
The rest is up to you.
Wanafunzi wa vyuo vya kati wameambiwa warudi nyumbani sababu ikiwa ni El nino, hadi hapo watakapotangaziwa kurudi, labda kuna kitu kingine kikubwa kinakuja na hatujawekwa wazi. Siku 90 zijazo zaweza zikawa ngumu sana, wanasema tuwe na akiba ya chakula, tusipuuze. Something big
220
BestHope retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
BestHope retweeted
Wakati sherehe za mashujaa wao zikipikwa na kuchochea, Ndivyo hadithi za mashujaa wangu zilizikwa na kupotea
29.10.2025 💔❤️🩹
Wana TOT hawatokusahau. Utaendelea kuwa kumbukumbu ya daima ya jinsi tulivyowapiteza wapendwa wetu tarehe 29 Oct 2025. Wote mpumzike kwa amani
BestHope retweeted
Mungu akubariki na kukulinda.
Mungu akuangazie nuru za uso wake na kukufadhili.
Mungu akuinulie uso wake na kukupa amani!


















