Natamani Nikae Mwaka Mmoja Bila Kutumia Mtandao wowote Wa Kijamii, Nisafiri tu niishi zamani , Niskilize Tu 89.0, 88.1, 95.3 😁
Zangu 10 hizi apa Nilikuwa Nikiskia Ivi Lazima Nijue Apo Class Lazima Watu wapigike 😁
1. Usichanganye Hizi Daftari na Hizi
2. Mwalimu amesema Hizi Daftari nisigawe Anakuja Kugawa mwenyewe
3.Funua Niliposahisha
4.Mmegoma Kumtaja?
5.Kitu Gani Kilikuwa Kigeni Ambacho sikufundisha
6.Asitoke Mtu Humu
7.Ukijibu Swali Unakaa
8.Kama Hujapata Mtihani wako Tangulia Staff
9.Kama Nimekuandikia See Me Songa Mbele
10.Fungua Faftari nione Ulipoandika kazi ya jana 😁
Hii Miaka Millennials walikuwa wanaambiwa Namba inayoishia na 666 Ikikupigia Usipokee Ukipokea Tu Unapoteza Fahamu Hapo Hapo , "Tuma ujumbe huu kwa Watu unaowapenda "
😁😁
Mnazisema Bangi Lakini Miaka 15 ijayo Taifa Litapoteza Vijana Wengi kwaajili ya Hivi Vidude wanangu 🫵
😁😁 Nna Hakika Hata Police Mwenyewe Alikuwa Anamuonea Jamaa Huruma Kwa Atakachoenda Kukutana Nacho 🙌🙌
4
198
Leo Nilikuwa Napita Mjini Insta Nikakuta Kumbe Davido Yupo apa +255, Sijafatilia Yupo Kwa Issue Gani,
Ila Kilichonishangaza Zaidi Ni kwamba Jamaa Anatumia Earphone Na Sio Earpod, Wakati Ni Juzi Tu Nimetoka Kutoa Kitita Cha Maana Kununua Soundcore Liberty 5 😁
Mjue Lissu Kwa Uchache 👇
Anaitwa Tundu Antiphas Lissu, Amezaliwa jan 1968, Singida, Alisoma Ilboru Sec, Kisha UDSM ,kisha Shahada ya Sheria LLM Warwivk UK mwaka 1996,
Aliwahi kuwa Rais Wa TLS, na 1990-1996 ndiyo Miaka Aliyozianza Harakati,Akawa Mwanachama Wa NCCR-Mageuzi, Akagombea Ubunge Mwaka 1995 lakini hakushinda
Mwaka 2004 alijiunga Na CHADEMA, Mwaka 2010 Akarematch na Akawa Mbunge Wa Singida , 7 september mwaka 2017 Alipigwa Risasi Dodoma na Kwenda Kutibiwa Nje Hali iliyofanya Kuchukuliwa kwa Kiti chake cha Ubunge ,
2020 alirudi Nchini na Aliteuliwa kugombea Urais Na Hakushinda, Mwaka 2025 Alishinda Kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa , Nyuma Kidogo Julai 2017 alishtakiwa kwa Kesi ya Uhaini Lakini Alishinda , Mwaka 2025-2026 alishtakiwa Kwa Kesi Ya Uhaini Akafanikiwa Kushinda Kesi Hiyo na Kukutwa na Hatia ya Kesi ya Uchochezi na kuhukumiwa Miaka 4 Jela
Aaah Qbbk Kumbe Bookmark Ndo History kidogo Ningeshindwa Kuzitama Video za Kumbu kumbu kwenye Rununu yangu 😂😂
Leo Pale Mjini YouTube nimekutana Na Debate Kuhusu Dini za Wazungu na Dini za Waafrica kilichonichosha zaidi Ni Kwamba Pande zote Mbili Walikuwa ni Waafrica Pande Moja kama Watetezi wa Wazungu
Nikakumbuka Ngoma Moja Kutoka kwenye Redemption Song ya Bob Marley,
"Emancipate yourselves from mental slavery"
Akisisitiza Afrika Iamke🫵 Kabla Hata Sijasearch App ya Spotify ilipo Ili Nirudie Kusikiliza Hii Nyimbo ya Bob Nikajiuliza Africa Tunataka Tuamke Tuende Wapi ?
Labda Tuamke afu Tulale Tena 😁 Maana Kama Mtu anaweza Kupiga Hela za Mradi wa Barabarani alafu yeye akaenda Kununua Gari Ambayo Njia ya kupita Hana!!
Bado miezi 2 tufike 2027, Nikitaka Kutoa Story Kuhusu Mwaka 2016 Hiyo Ni story ya Miaka 10 Iliyopita , kama Umezaliwa Mwaka 1990 Umebakiza Miaka 14 tu uwe Na Miaka 50, Mwaka 2007 ni Mbali kuliko mwaka 2040,
Muda Unakwenda Sana!, Punguza Kusubiri wakati Sahihi Ndipo Uanze , Anza Sasa Hivi anza Kidogo Kidogo 🫵
1
6
317















