Ahmad Issa Michuzi (@MichuziJr) header
Ahmad Issa Michuzi (@MichuziJr) profile picture

Influencer

Dar es salaam
Joined June 2009
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, kuelekea Entebbe nchini Uganda kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa,leo Novemba 18, 2026.
99
Hii ndio Zaidi, kaa mkao wa kula. Wiki ijayo Vodacom wana jambo kubwa, haachwi mtu hapa.
53
Hii ndio Zaidi, kaa mkao wa kula. Wiki ijayo Vodacom wana jambo kubwa, haachwi mtu hapa.
101
KUELEKEA SAFARI YA MARIDHIANO.
1
143
RAIS SAMIA AKUTANA NA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa katika kikao kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, Novemba 16, 2026.
3
1
2
155
SHETTA: MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIANCHI YAENDE SAMBAMBA NA AFYA NA AJIRA Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta), amesema hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinapaswa kwenda sambamba na kuboresha afya ya umma, kuunda ajira zenye staha na kuimarisha ustahimilivu wa miji dhidi ya changamoto mbalimbali. Amesema hayo akieleza msimamo wa Jiji la Dar es Salaam, akibainisha kuwa kama mojawapo ya miji inayokua kwa kasi barani Afrika, ni muhimu kuhakikisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inaleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaofanyika Antalya, nchini Uturuki.
1
1
83
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipongezwa mara baada ya kuongoza mjadala kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika katika Mkutano wa Ngazi ya Juu uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa COP31, Novemba 12, 2026, katika Kituo cha Mikutano cha ANFAŞ Antalya Expo Center, nchini Uturuki. @suluhu_hassan @ikulumawasliano #cop31
1
125
POSTA TANZANIA KUWAPIMA MAMENEJA KWA MATOKEO, WASIOTIMIZA MALENGO KUWAJIBISHWA Shirika la Posta Tanzania limeweka msisitizo mpya katika uwajibikaji kwa kutangaza kuwa utendaji wa mameneja wa mikoa na viongozi wengine utapimwa kwa kuzingatia matokeo ya biashara, ubora wa huduma na uwezo wa kutumia fursa zilizopo kukuza shirika hilo. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Novemba 12, 2026, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mameneja wa mikoa, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo, amesema viongozi watakaoshindwa kutimiza majukumu yao watawajibishwa baada ya tathmini ya utendaji, akisisitiza kuwa hakuna kiongozi atakayebaki nje ya mchakato huo, wakiwemo wa makao makuu. Mbodo amesema tathmini hizo zitazingatia matokeo ya kila eneo kwa haki, huku watendaji wanaofanya vizuri wakitambuliwa na maeneo yenye changamoto yakifanyiwa uchambuzi kwa lengo la kuboresha utendaji. Akitolea mfano wa mafanikio, ametaja Mkoa wa Morogoro ambao umepata fursa kubwa ya biashara ya usafirishaji wa vifurushi, kiasi cha kukabiliwa na upungufu wa magari kutokana na ongezeko la mahitaji. Amesema meneja wa mkoa huo ameweka lengo la kusafirisha vifurushi 5,000, hivyo kuitaka menejimenti kutoa rasilimali zinazohitajika. Katika hatua nyingine, Mbodo amesema Tanzania imepiga hatua katika ushindani wa kimataifa kwa kushika nafasi ya 66 duniani na ya nne barani Afrika katika tathmini ya Umoja wa Posta Duniani (UPU), huku akieleza kuwa shirika hilo linaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha nafasi yake na kuwa kinara wa huduma za posta barani Afrika. Amewataka mameneja kutumia mafunzo hayo kuboresha usimamizi wa biashara, matumizi ya rasilimali, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wateja, akisisitiza kuwa ukuaji wa Shirika la Posta Tanzania ni jukumu la kila mtumishi.
99
SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA KUHARAKISHA MAGEUZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu kuharakisha mageuzi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania, hususan katika shule na vituo vya afya, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa COP31 katika ukumbi wa ANFAŞ Antalya Expo Center, Antalya, Uturuki, Novemba 11, 2026. Mkutano huo uliandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Sustainable Energy for All (SEforALL).
1
1
141
♦️*POSTA YAENDELEA KUIUNGANISHA TANZANIA KWA USAFIRISHAJI, YASHIRIKI UZINDUZI WA XERIN MARKET*♦️ Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeendelea kuimarisha nafasi yake kama mdau muhimu na bingwa wa usafirishaji na usambazaji wa bidhaa nchini, baada ya kushiriki katika uzinduzi rasmi wa jukwaa la biashara, Xerin Market, hatua inayolenga kuunganisha biashara na huduma za usafirishaji ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi. Uzinduzi huo uliofanyika, Novemba 11, 2026, Kariakoo Jijini Dar es Salaam, ukihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. Ephraim Mafuru, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, huku Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Posta Bw. Ferdinand Kabyemela akimwakilisha Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania. Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Kabyemela amesema, mafanikio ya kibiashara hayaishii katika kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi kupitia teknolojia pekee, bali yanategemea pia uwepo wa mfumo madhubuti wa usafirishaji na usambazaji wa bidhaa unaotolewa na Shirika la Posta. Uzinduzi wa Xerin Market unaongeza fursa ya kuunganisha wafanyabiashara wa Kariakoo na maeneo mengine nchini na masoko mapana zaidi, huku ushirikiano na Posta ukiweka msingi wa kuimarisha huduma za usafirishaji na usambazaji wa bidhaa kwa wateja. Kupitia ushiriki wake katika jukwaa hilo, Shirika la Posta Tanzania linaendelea kuthibitisha umuhimu wake katika sekta ya usafirishaji kwa kutumia miundombinu yake kuunganisha watu, biashara na fursa, huku likiendelea kuweka mbele utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
1
1
80
Alichozungumza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwenye Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), Antalya Expo Center nchini Uturuki, leo Novemba 11, 2026.
1
77
RAIS SAMIA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA COP31 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Antalya Expo Center, nchini Uturuki, Novemba 11, 2026.
1
1
84
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mhe. António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) (kushoto) pamoja na Mhe. Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki (kulia), baada ya kuwasili ANFAŞ Antalya Expo Center nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), tarehe 11 Novemba, 2026. @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano
62
RAIS SAMIA AWASILI ANTALYA, UTURUKI KUSHIRIKI MKUTANO WA COP31 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili Jijini Antalya nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
1
195
RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUSHIRIKI COP31 UTURUKI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Novemba 10, 2026, kabla ya kuondoka kuelekea Antalya, Uturuki, kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
1
2
97
RAIS SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA COP31,UTURUKI.
94
MIGIRO ACHAGULIWA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VYAMA VYA SIASA BARANI AFRIKA (APPI) KANDA YA AFRIKA MASHARIKI.
4
1,047
📌 *POSTA YATOA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA PMI TANZANIA 2026* Shirika la Posta Tanzania limeendelea kuonesha uwezo na uzoefu wake katika usimamizi wa miradi kwa kutoa mafunzo kupitia mjadala wa jopo kuhusu Ofisi za Usimamizi wa Miradi katika Taasisi za Umma, kwenye Mkutano wa Mwaka wa PMI Tanzania Project Management Week & Annual Conference 2026. *POSTA DELIVERS BETTER!* #PostaMorogoro #PostaNiZaidiyaBarua #PostaDeliversBetter #PMITanzania2026
1
3
341