Ahmad Issa Michuzi (@MichuziJr) header
Ahmad Issa Michuzi (@MichuziJr) profile picture

Influencer

Dar es salaam
Joined June 2009
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Ninawatakia nyote kheri katika maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kwa miaka 62 tumeendeleza dhamira ya msingi ya Mapinduzi ya kujenga jamii ya watu huru, yenye utu, yenye maendeleo, umoja, haki, amani na mshikamano. Sote tunao wajibu wa kuendelea kuzilinda tunu hizi na kuzirithisha kwa vizazi vijavyo, kama tulivyorithi toka kwa waasisi wetu.
9
133
17
484
34,482
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Mapema leo katika kazi jijini Dodoma ambapo nchi yetu imeandika historia kwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu. Uamuzi huu wa kihistoria wa kuboresha sera na muundo wa elimu yetu unakusudia kulipa Taifa letu vijana wenye elimu bora zaidi, wanaojiamini zaidi, na wenye nyenzo stahiki kushindana kikanda na kimataifa. Kazi ya msingi ya ujenzi wa miundombinu inayobeba utekelezaji wa sera na mabadiliko haya inaendelea, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 tumejenga shule mpya za msingi 1,649, shule mpya za sekondari 1,042, vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo awali hazikuwa navyo. Nimeelekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mabadiliko haya ili yaweze kuleta manufaa tunayokusudia. Utekelezaji huu uende sambamba na kupitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahili kama mama wa taaluma zote duniani.
231
254
15
1,027
79,927
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Hongera kwa Klabu ya Yanga kwa ushindi dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Nawatakia kila la kheri katika michezo iliyosalia kwenye mashindano haya. Endeleeni kutupa burudani na kufanya kazi njema ya kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa.
343
444
28
3,689
116,279
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Mama yetu, Mama Maria Nyerere leo anapotimiza umri wa miaka 94. Namshukuru kwa busara zake na upendo wake. Tumuombee furaha, amani na siha njema.
290
302
7
2,090
86,071
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Kheri ya Miaka 63 ya Uhuru kwetu sote. Tutumie siku hii njema kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua kubwa tunazoendelea kupiga kimaendeleo kama Taifa. Tujivunie, na kwa pamoja tuendelee kufanya kazi ya kuzilinda na kuzitunza tunu za amani, umoja na mshikamano ambazo ndizo nguzo za mafanikio yetu.
488
387
39
1,817
161,369
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Kila la kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Nne mnapoanza Mtihani wa Kuhitimu (CSEE) leo. Nawaombea utulivu na mafaniko katika hatua hii muhimu ya kujiandaa kushiriki vyema kwenye nguvu kazi ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla. Mafanikio yenu katika hatua hii yatakuwa pia faraja kwa waalimu, wazazi na Watanzania wote ambao kupitia ulipaji kodi na utunzaji wa amani na utulivu wa nchi yetu wanaiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza mipango tunayojiwekea, ikiwemo kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi Kidato cha Sita, na kazi mpya tuliyoanza ya kuboresha mfumo wetu wa elimu ili uendane na mazingira na mahitaji ya sasa. Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia.
281
288
16
2,560
165,008
Ahmad Issa Michuzi retweeted
On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency @realDonaldTrump, President-elect of the United States of America on your election victory. Mr. President-elect, you have my best wishes. I am looking forward to working together to strengthen the bilateral relations between Tanzania and the United States.
811
662
71
6,422
505,100
Ahmad Issa Michuzi retweeted
To His Excellency Duma Boko, President-elect of the Republic of Botswana; on behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I convey my heartfelt congratulations on your victory in the 2024 Botswana general election. I also salute His Excellency President Mokgweetsi Masisi and the Botswana Democratic Party (BDP) leadership for their commitment to ensuring a smooth transition. Your Excellency, President-elect, we look forward to working closely with you to further strengthen our long-standing bilateral ties.
364
569
57
3,664
234,845
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Kwaheri, Jenerali. Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Makamanda, wapiganaji wastaafu, wapiganaji walio katika utumishi, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wetu, mpendwa wetu, mwalimu, mshauri na kiongozi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake ya miaka 104, ambapo miaka 46 kati ya hiyo ameitumikia nchi yetu kwa weledi, umahiri, kujituma, ushujaa, nidhamu na kwa mafanikio ya hali ya juu, akiishi kiapo chake cha kuwa tayari kuutoa uhai wake ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Ametuachia mfano bora wa utumishi wa umma utakaoendelea kuwa mwanga ndani na nje ya Majeshi yetu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
305
297
23
2,123
155,072
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali za barabarani zilizotokea katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro na kusababisha vifo na majeruhi. Nawapa pole wafiwa wote, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawaombea marehemu wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka. Tunapoelekea mwishoni mwa mwaka, nawasihi watumiaji wote wa barabara kuongeza umakini. Nimeziagiza mamlaka zote husika kuongeza umakini katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani. Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina.
213
160
7
992
116,608
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Tamu sana Nzuri mno Tunatuma hadi nnje ya Nchi 🥰 #BEBES Peanut Butter . Mcheki tajir DorothNengai umpe oda Nimezipa 21km chap Jpili nitazipa 42 km 😝 Kimbia kwa mwendo wako
2
26
37
5,235
Ahmad Issa Michuzi retweeted
On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency Paul Kagame, on being re-elected as the President of the Republic of Rwanda. I look forward to continue working with you in fostering the relations between our two countries and in the pursuit of East Africa’s unity and prosperity.
313
994
52
5,795
238,652
Ahmad Issa Michuzi retweeted
The #ITAC2024 discussion will be on the exploration of public procurement systems’ transparency and accountability mechanisms to enhance effectiveness and efficiency in the public procurement lifecycle. Register now to join the conversation! itac.wajibu.or.tz/
9
1
7
1,507
Ahmad Issa Michuzi retweeted
🇹🇿♥️🇰🇷
499
1,006
268
4,152
301,672
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Pongezi za dhati kwa Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa, Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Kuchaguliwa kwako katika nafasi hii ya uchungaji kwa Kanisa Katoliki nchini ni matokeo ya imani na matarajio ya Kanisa kwa utumishi wako. Nanukuu maneno mawili toka katika Biblia Takatifu kwenye Injili ya Yohana 19:28, “...Naona kiu” ambayo pia uliyachagua kuwa kaulimbiu yako ya Uaskofu. Katika utumishi huu nakuombea kiu ya kuendelea kufanya kazi ya kujenga Kanisa kwenye misingi ya upendo, haki, kweli, kujali masikini, umoja, amani, mshikamano, utu na kuhudumia jamii na Watanzania kwa ujumla, ndani na nje ya Kanisa Katoliki. Nakutakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu akushike mkono na kukuongoza.
279
200
7
1,430
87,707
Ahmad Issa Michuzi retweeted
On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency Cyril Ramaphosa, on being once again entrusted by the people of the Republic of South Africa with a responsibility to lead them as their President. Tanzania and South Africa are sister Republics. I am looking forward to continue working with you in further strengthening the deep fraternal bonds and historical ties between our two countries and peoples.
234
312
8
2,252
118,916
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Nawatakia nyote kheri tunapoadhimisha Miaka 60 ya Muungano wetu. Hii ni tunu yetu sote, matokeo ya kazi ya kila Mtanzania kuanzia waasisi wetu mpaka sasa. Tumejenga nyumba imara ya Tanzania katika misingi ya utu, udugu na uanamajumui wa Afrika hatua kwa hatua, chini ya kila awamu ya uongozi. Zawadi pekee tunayoweza kuwapa waasisi wa Muungano huu ni kuulinda na kuishi maono yao haya makubwa. Sote ni mashahidi wa hatua kubwa tulizopiga kimaendeleo katika kipindi cha Miaka 60. Tuna kila sababu ya kuendelea kujivunia na kuulinda Muungano huu wa kipekee uliotokana na uamuzi wetu wenyewe. Katika kuuendeleza, hatuna budi kutekeleza falsafa ya Maridhiano, Ustahamilivu, Mageuzi na Kujenga Upya nchi yetu ili kudumisha amani na utulivu, nguzo muhimu kwa ustawi na uimara wa Taifa letu. Kheri ya Kumbukizi ya Siku ya kuasisiwa Tanzania yetu. Kheri ya Miaka 60 Tanzania yetu. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika.
322
385
15
2,750
127,056
Ahmad Issa Michuzi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kenya, Jenerali Francis Omondi Ogolla na wanajeshi wengine tisa katika ajali ya helikopta iliyotokea leo katika Kaunti ya Elgeyo-Marakwet. Natuma salamu za pole kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Mheshimiwa @WilliamsRuto, wananchi wote wa Kenya, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa wote waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hiyo. Poleni sana. Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina.
894
1,799
59
13,950
788,612
Ahmad Issa Michuzi retweeted
23
20
11
94
10,738
Ahmad Issa Michuzi retweeted
On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency, President Vladimir Putin on being re-elected as the President of the Russian Federation. We are looking forward to continue working together to strengthen the bilateral relations between Tanzania and Russia.
576
1,046
88
7,746
467,963