Prosper Masau retweeted
Sehemu ya hotuba yangu leo nikiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, nimewaagiza viongozi kushughulikia changamoto za wananchi na kutekeleza majukumu yao kikamilifu bila kusubiri maelekezo au ziara za viongozi wa kitaifa.
Prosper Masau retweeted
Hivi majirani Mnajua kama ukiachana na AFCON, mwakani Pia Tanzania ni mwenyeji wa Miss World? Mwaka huu pia Serengeti ni Mwenyeji wa Tuzo za Dunia za Utalii?
Prosper Masau retweeted
TAMKO LA TLS KUHUSU HUKUMU YA TUNDU LISSU
TLS imetoa tamko rasmi kuhusu hukumu ya Mhe. Tundu Lissu
Kusoma tamko lote, tembelea: tls.or.tz/uploads/1795760938…
#tls #UtawalaWaSheria #Tanzania
Prosper Masau retweeted
Shauri la Tito Elia Magoti & Another v. Minister for Communication and Information Technology & Others, Miscellaneous Civil Cause No. 2378 of 2026, \[2026\] TZHC 7037, lililotolewa tarehe 24 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania ilichunguza uhalali wa kikatiba wa uamuzi wa Serikali kuzuia upatikanaji wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) nchini Tanzania tarehe 20 na 21 Mei 2025. Waombaji walidai kuwa hatua hiyo ilikiuka haki zao za kikatiba, hususan uhuru wa kujieleza chini ya Ibara ya 18, haki ya kupata taarifa, uhuru wa kukusanyika na kushirikiana chini ya Ibara ya 20(1), pamoja na haki nyingine za msingi.
Kwa upande mwingine, Serikali ilitetea hatua hiyo kwa misingi ya kulinda usalama wa umma, jamii na maadili, ikitegemea Kanuni za 16 na 19(b) za Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni), za mwaka 2020. Mahakama ilisisitiza kuwa ingawa haki za msingi zinaweza kuwekwa mipaka chini ya Ibara ya 30 ya Katiba, mipaka hiyo lazima iwe na msingi wa kisheria, iwe na lengo halali na izingatie uwiano kati ya hatua inayochukuliwa na lengo linalokusudiwa.
Katika uamuzi wake, Mahakama ilibaini kuwa Kanuni ya 19(b) inaipa TCRA mamlaka ya kuondoa au kuzuia upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kisheria, lakini haitoi mamlaka ya kuzuia mtandao mzima wa kijamii. Hivyo, Serikali ilivuka mipaka ya mamlaka yake ya kisheria kwa kuzuia upatikanaji wa jukwaa zima la X bila kuwa na msingi mahsusi wa kisheria.
Mahakama ilitangaza hatua hiyo kuwa kinyume cha Katiba na kuamuru vizuizi vyote vilivyowekwa viondolewe mara moja ili kurejesha upatikanaji wa X bila vikwazo, bila kuathiri mamlaka halali ya TCRA ya kudhibiti maudhui yaliyokatazwa.
Prosper Masau retweeted
Sigue el asombro con las imágenes del Cristo Redentor de Río de Janeiro
Emergiendo entre las nubes con los brazos abiertos. 🙌
Prosper Masau retweeted
🇧🇷 BREATHTAKING: A rare cloud cascade surrounds Brazil’s Christ the Redeemer, pouring down the mountain like a heavenly waterfall.
God’s creation is truly remarkable. ✝️
Prosper Masau retweeted
Photographers capture stunning footage of the Christ the Redeemer statue floating above the clouds atop Corcovado Mountain in Brazil.
Remarkable.
Prosper Masau retweeted
This is CHRIST THE REDEEMER statue in Rio de Jeneiro, Brazil 🇧🇷 I’m blessed to have seen this place myself.
Prosper Masau retweeted
Tumepokea …… Asante sana Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Ahadi yetu…..juhudi zinaendelea. Chalinze inakushukuru kwa mafanikio makubwa zaidi ya hayo.Katika Miaka 6 ya Uongozi wa Awamu ya Sita katika sekta ya Afya Umefanikisha Ujenzi wa HOSPITALI ya Wilaya 1 , Vituo vya Afya 4 na Zahanati katika Vijiji Vyetu 15, Magari ya Wagonjwa 6 na ahadi ya kununua 3 katika Miaka Mitano hii.
#AfyaChalinze #KaziInaendelea
Prosper Masau retweeted
Watu wenye busara hufanya matendo makubwa ya upendo kimya kimya bila kutangaza wala kutafuta sifa
Prosper Masau retweeted
Kipindi kama hiki, ndio ilitakiwa mitandao iliyofungwa, iachiwe. Majukwaa ya kidigitali yawe huru.
A new HQ. A new partnership. Another milestone for #TotalEnergiesAFCON2027! 🇹🇿✨
Take a look back at the inauguration and the signing ceremony with Official Competition Sponsor, Tanzania Tourist Board. 🌍
Prosper Masau retweeted
Wait Kenya! Muone namna ambavyo Tanzania tutakavyotumia AFCON 2027 kutangaza utalii wetu kimataifa. I’m sure hamtapenda tutakachokifanya! 😁
Prosper Masau retweeted
Salamu.
Kwa baraka zake, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote aliyonijaalia yanayoonekana na yasiyoonekana.
Nimepokea kwa unyenyekevu mkubwa uhamisho wangu kutoka nafasi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo & Msemaji Mkuu wa Serikali kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Kwa dhati ya moyo wangu namshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini katika utumishi ndani ya Serikali yake ya Awamu ya Sita. Ni dhamana kubwa na yenye maana kubwa kwangu na familia yangu.
Asubuhi hii nilipoamka Mwanangu (Daktari Tarajali) kaniuliza “Hey, Gentleman, is everything alright?” Nikamwambia very fine, akaniambia “Keep it burning” halafu huyoo kaenda zake hospitali kuhudumia wagonjwa 😂😂.
Nawashukuruni nyote, wadau wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ushirikiano mkubwa mlionipa katika majukumu yangu ya Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nawashukuru sana watazamaji, wasikilizaji na wasomaji wote katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambako shughuli zangu nyingi zimekuwa huko. Nawashukuru wamiliki wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, nyie Waandishi wa Habari ni ndugu zangu kabisa, mimi na nyinyi mpaka watuue😜😜.
Kama nilivyomjibu mwanangu, niko sawa, niko tayari kwa kazi na niko timamu kuitumikia dhamana mpya niliyopewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nawaombeni tuendelee kushirikiana katika kulijenga Taifa letu. Tuna Tanzania moja tu na sisi ndio Watanzania wenyewe wa kuijenga au kuibomoa. Tuchague kuijenga.
Nawashukuru viongozi na watumishi wote wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali na taasisi zote za Wizara kwa ushirikiano na upendo mkubwa tuliokuwa nao. Endelezeni utamaduni huu tulioujenga pamoja.
Nawatakia kheri Bw. Abdallah Hassan Mitawi aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Dkt. Ayub Rioba Chacha aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali. Mungu awasimamie daima.
Karibuni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
#KaziIendelee
Prosper Masau retweeted
AFCON 2027 is an economic opportunity East African youth cannot afford to overlook. Beyond football, there are opportunities in tourism, hospitality, transport, construction, technology, marketing, entertainment & trade. Let us prepare early, build partnerships & position ourselves to benefit. When the final whistle blows, we must have more than memories, businesses established, jobs created, income generated & skills gained. AFCON must leave a lasting economic legacy for East Africa.
Prosper Masau retweeted
“Every time you hold yourself to a higher standard, you raise the bar for what is possible for everyone around you. That is the power you hold, so you need to use it wisely.” ~ @PaulKagame #YouthConnekt2026
Prosper Masau retweeted
The meaning of the expression “an unarmed and disarming peace” is closely linked to the words of the Risen Lord: “Peace be with you” (Jn 20:19, 21). The peace to which we all aspire, which has no need of weapons and is indeed capable of disarming armies and hearts, is therefore the peace of Christ and is a gift from God. vatican.va/content/leo-xiv/e…
Prosper Masau retweeted
Leo jijini Dar es Salaam nimepata heshima ya kufungua Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe. Mkutano huu unalenga kuweka mikakati ya kuboresha huduma za afya na lishe ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika ifikapo mwaka 2030 na kufikia malengo ya Sifuri Tatu.
Kazi kubwa tuliyofanya ya kujenga vituo vya kutolea huduma za afya kila kona ya nchi, kuajiri watumishi wa afya, na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeiwezesha nchi yetu kupiga hatua kubwa katika kutimiza malengo hayo. Ili kuongeza kasi ya utekelezaji, leo nimeingia mkataba na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara kuhusu usimamizi wa masuala ya afya na lishe katika maeneo yao.
Ninaziagiza Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mikataba hiyo. Ninawakumbusha kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora za afya bila kujali anapoishi, kipato chake au hadhi yake.








































