Christian Bwaya retweeted
Umewahi kusikia hoja za mtu ukaishia kuhoji elimu yake? Unamsikiliza unajiuliza hivi ni kweli huyu haelewi anachozungumza? Hofu huzuia kufikiri. Hofu ni hali ya kujisikia hauko salama wala huru. Ukiangalia mchoro huu unaona, kimaumbile, huwezi kutumia akili zako vizuri kudadisi mambo ikiwa hujisikii salama. Ndio maana ni muhimu ukiwa kiongozi uwekeze vya kutosha kuwafanya watu waamini wako salama ili wasitumie nguvu na muda mwingi kujihami kuliko kufikiri.
Lakini pia, huenda umewahi kujiuliza kwa nini mtu anaweza kutetea kitu anachojua vizuri kabisa kuwa hakina maana. Kwa nini wapenzi hupuuza viashiria vyote vya mienendo wanayokuja kuithibitisha baadae? Jibu lipo hapo hapo kwenye usalama wa kihisia.
Ukishakuwa na maslahi na mtu, kuna kitu unakihitaji kwake, ubongo wako una kawaida ya kukusaidia kutunza usalama wa mahusiano yenu kwa kufikiri kinachoendana na hisia zako—ndio maana kushauri watu waliopendana ni kujichosha.
Christian Bwaya retweeted
Umewahi kufikiri kwa nini unashindwa kusahau maumivu uliyowahi kupitia—mpenzi aliyekudhalilisha, bosi aliyekuonea, rafiki aliyekusaliti, au hata kuondokewa na mpendwa wako? Kwa nini huachi kukumbuka historia usiyotaka kuikumbuka? Nini ufanye ukitaka kusahau?
Kwanza kabisa, muhimu kuelewa namna ubongo wako unavyofanya kazi. Ubongo hung’ang’ania chochote kilichowahi kukuumiza. Hisia zetu huwa hazisahauliki. Kilichowahi kukupata kikakuumiza ubongo unatambua kuwa hiyo ni sehemu muhimu ya historia yako hata kama hukipendi. Ukijifanya kuukana ukweli ndio uharibu zaidi. Ubongo haupendi uongo. Kukukumbusha historia usiyoipenda ni wajibu wake kimaumbile kukulinda na uwezekano wa kukuathiriwa na hatari hiyo hiyo.
Wengi wetu hupambana kujisahaulisha maumivu kwa kujifanya hatuujui ukweli. Tunaugeuza simulizi. Tunageuza kibao ili kujinasua na hatia, majuto na aibu. Tunachana picha za wapenzi wetu wastaafu tena saa nyingine tukijiapiza kulipiza kisasi. Tunafuta namba za wanaotuudhi na wakati mwingine kuhama mtaa. Tunatumia nguvu kubwa kupambana na vipande vya maisha yetu vyenye simulizi za maumivu. Lakini kadiri tunavyojitahidi kuchana-chana kurasa hizo za aibu ndivyo ubongo unavyozidi kutukumbusha uongo tunaoutumia kujidanganya.
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa pale mtu unapoacha kujidanganya na kuukabili ukweli mchungu, pale unapoanza kukumbuka kile kinachokuumiza, ubongo unakuheshimu na kukusaidia kuachilia maumivu uliyonayo. Kama mzaha fulani hivi lakini huo ndio ukweli kuwa ubongo unakusubiri uwe mkweli kwa nafsi yako uukubali ukweli hata kama unakuumiza na kukufedhehesha.
Sema unavyojisikia. Elezea hisia zako waziwazi bila kificho hata kama kwa kufanya hivyo inakuwa kama unajitonesha kidonda kibichi. Kama huwezi kusema basi jaribu kuandika. Tafuta mahali pa kuuandika uchungu unaokusumbua. Ukiweza kupata maneno sahihi yanayobeba uchungu wako ubongo unaanza kukupumzisha kwa kukutengenezea maelezo yanayohitimisha simulizi hilo linalokuumiza. Shida yetu huwa tunafikiri kukwepa hisia ngumu kunasaidia na tusichojua ni kwamba kadri tunavyokwepa ndivyo tunavyousumbua ubongo kuendelea kuona hatari.
Kwa muhtasari kabisa unapona kwa kurudia rudia kinachokuumiza. Uvae ujasiri kukubali kuwa uliumia. Kiri kuwa ulikosea. Kiri kuwa kuna mtu ulimiuumiza. Kiri kuwa kuna mtu uliharibu maisha yake. Ubongo ukishagundua kumbe umeshakubali maumivu yako unaacha kuyaona kama hatari na kukusaidia kuhariri kumbukumbu husika kwa namna isiyoendelea kukuumiza zaidi. Kwa maana nyingine, kadiri unavyojipa ruhusa ya kuyakabili maumivu yako bila kuyaogopa, unauruhusu ubongo kuboresha kile unachokikumbuka. Husahau kwa kusahau. Unasahau kwa kukumbuka.
Christian Bwaya retweeted
Kuna wakati maumivu ya kihisia huwa makali kiasi kwamba kila unapoyakumbuka inakuwa kama kubandua ganda la kidonda kibichi. Unafanya nini katika hali kama hii? Je, unajisahaulisha na kuiaminisha akili yako kwamba hukuumia? Tumeona, kwa hakika, ubongo huwa haudanganyiki. Je, unakilazimisha kidonda kukauka kabla ya wakati kwa kubeza maumivu yako mwenyewe au ya mtu uliyemwuumiza? Hii ni sawa na kutia chumvi kidonda.
Hatua ya kwanza kuchukua ni kutulia kidogo pasipokufanya jitihada zozote za kuufukia ukweli. Sema unavyojisikia bila kuigiza ‘muujiza wa uponyaji’ usiokuwepo. Kuna tofauti kubwa kati ya kujifanya ‘maisha yanaendelea kama kawaida’ wakati unajua fika umeumia. Kuna tofauti kubwa kati ya imani na kujidanganya. Unapokiri kuwa “nimeumia” haimaanishi huna imani. Unaweza kukabiliana na uhalisia bila kupoteza matumaini.
Unapokabiliana na uhalisia, hata hivyo, unaweza kuanza kujisikia fedheha ikibisha hodi, “Kwa nini imekuwa hivi?” Fedheha inanyonya ujasiri wako kwa kukusanya ushahidi kuwa umeisha. Katika mazingira haya inasaidia kutenganisha uhalisia (wa kilichotokea) na kujilaumu (kujizomea). Unaposema “Sikuliona hili likitokea na sikuwa nimejiandaa na maumivu ya kuachika” ni tofauti na kusema “Nilikuwa mjinga sana kukubali kuonewa kwa muda mrefu.” dhidi yako mwenyewe. Lugha unayotumia inaweza kukusaidia kujizomea na huo ukawa mwanzo wa kutafuta kaburi la kuzika kumbukumbu zitakazokutesa kwa miaka mingi.
Kadhalika, kupata mtu unayemwamini akusaidie kuukabili ukweli unaokuumiza inaweza kuwa tiba. Tafuta mshunuzi, mnasihi au hata mtu mwenye hekima akusaidie kubeba mzigo unaokuzidia. Wengi wetu tunaishi na chuki, visasi na maumivu makali kwa vile hatukutafuta msaada wakati kidonda ni kibichi. Tunaendelea na maisha yetu na kutembea barabarani kama watu wasio na tatizo. Tunapiga picha zenye kuonesha nyuso za matumaini lakini moyoni tunavuja damu. Tunapoelemewa na maumivu tunachagua kuwageuzia kibao watu tukifikiri itatusaidia kusahau maumivu yetu.
Kujiuguza na kupona majeraha yako, hata hivyo, haimaanishi ‘ujimalize’ kwa kusema kila kitu kwa kila kitu kwa mtu anayelazimisha kujua unachopitia. Uponyaji wa kweli unamaanisha kuacha kujidanganya kwamba ‘maisha yanaendelea’ na kutokuingia kwenye mtego mbaya wa kujisahaulisha kilichokuumiza. Hatuponi kwa kujifanya hatukuumia. Hatuponi kwa kujidanganya kuwa tumepona kabla ya wakati.
Hadharani una furaha, sirini unalia.
Hadharani ni maarufu, sirini ni mpweke.
Hadharani ni jasiri, sirini mnyonge.
Hadharani una hekima, sirini ni mjinga.
Hadharani ni mwema, sirini ni mwovu.
Hadharani ni mcha Mungu, sirini ni mshirikina.
Hadharani umeridhika, sirini una roho mbaya.
Hadharani una utu, sirini ni mnyama.
Hadharani unapenda familia, sirini umeitelekeza.
Hadharani ni mwaminifu, sirini unachepuka.
Hadharani una bidii, sirini ni mzembe.
Hadharani umefanikiwa, kwa siri huna uhakika na kesho.
Tunapenda kuonekana na ukamilifu tusiokuwa nao. Tunapenda kutambulika kwa mafanikio tunayojua hayapo. Tunajigombanisha na ukweli wa sirini tusiothubutu kuusema waziwazi. Matokeo yake, ‘ukamilifu’ huu unatutumikisha, unatunyanyasa na kututengenezea maumivu mengi ya kihisia tunayoona aibu kuyatafutia tiba.
Tusiwanyime watoto fursa ya kujisikia aibu wanapokosea. Utu wa mtu, kwa kiasi kikubwa, unategemea uwezo wake wa kujisikia aibu na hata kufedheheka.
Kuna wakati maumivu ya kihisia huwa makali kiasi kwamba kila unapoyakumbuka inakuwa kama kubandua ganda la kidonda kibichi. Unafanya nini katika hali kama hii? Je, unajisahaulisha na kuiaminisha akili yako kwamba hukuumia? Tumeona, kwa hakika, ubongo huwa haudanganyiki. Je, unakilazimisha kidonda kukauka kabla ya wakati kwa kubeza maumivu yako mwenyewe au ya mtu uliyemwuumiza? Hii ni sawa na kutia chumvi kidonda.
Hatua ya kwanza kuchukua ni kutulia kidogo pasipokufanya jitihada zozote za kuufukia ukweli. Sema unavyojisikia bila kuigiza ‘muujiza wa uponyaji’ usiokuwepo. Kuna tofauti kubwa kati ya kujifanya ‘maisha yanaendelea kama kawaida’ wakati unajua fika umeumia. Kuna tofauti kubwa kati ya imani na kujidanganya. Unapokiri kuwa “nimeumia” haimaanishi huna imani. Unaweza kukabiliana na uhalisia bila kupoteza matumaini.
Unapokabiliana na uhalisia, hata hivyo, unaweza kuanza kujisikia fedheha ikibisha hodi, “Kwa nini imekuwa hivi?” Fedheha inanyonya ujasiri wako kwa kukusanya ushahidi kuwa umeisha. Katika mazingira haya inasaidia kutenganisha uhalisia (wa kilichotokea) na kujilaumu (kujizomea). Unaposema “Sikuliona hili likitokea na sikuwa nimejiandaa na maumivu ya kuachika” ni tofauti na kusema “Nilikuwa mjinga sana kukubali kuonewa kwa muda mrefu.” dhidi yako mwenyewe. Lugha unayotumia inaweza kukusaidia kujizomea na huo ukawa mwanzo wa kutafuta kaburi la kuzika kumbukumbu zitakazokutesa kwa miaka mingi.
Kadhalika, kupata mtu unayemwamini akusaidie kuukabili ukweli unaokuumiza inaweza kuwa tiba. Tafuta mshunuzi, mnasihi au hata mtu mwenye hekima akusaidie kubeba mzigo unaokuzidia. Wengi wetu tunaishi na chuki, visasi na maumivu makali kwa vile hatukutafuta msaada wakati kidonda ni kibichi. Tunaendelea na maisha yetu na kutembea barabarani kama watu wasio na tatizo. Tunapiga picha zenye kuonesha nyuso za matumaini lakini moyoni tunavuja damu. Tunapoelemewa na maumivu tunachagua kuwageuzia kibao watu tukifikiri itatusaidia kusahau maumivu yetu.
Kujiuguza na kupona majeraha yako, hata hivyo, haimaanishi ‘ujimalize’ kwa kusema kila kitu kwa kila kitu kwa mtu anayelazimisha kujua unachopitia. Uponyaji wa kweli unamaanisha kuacha kujidanganya kwamba ‘maisha yanaendelea’ na kutokuingia kwenye mtego mbaya wa kujisahaulisha kilichokuumiza. Hatuponi kwa kujifanya hatukuumia. Hatuponi kwa kujidanganya kuwa tumepona kabla ya wakati.
Umewahi kufikiri kwa nini unashindwa kusahau maumivu uliyowahi kupitia—mpenzi aliyekudhalilisha, bosi aliyekuonea, rafiki aliyekusaliti, au hata kuondokewa na mpendwa wako? Kwa nini huachi kukumbuka historia usiyotaka kuikumbuka? Nini ufanye ukitaka kusahau?
Kwanza kabisa, muhimu kuelewa namna ubongo wako unavyofanya kazi. Ubongo hung’ang’ania chochote kilichowahi kukuumiza. Hisia zetu huwa hazisahauliki. Kilichowahi kukupata kikakuumiza ubongo unatambua kuwa hiyo ni sehemu muhimu ya historia yako hata kama hukipendi. Ukijifanya kuukana ukweli ndio uharibu zaidi. Ubongo haupendi uongo. Kukukumbusha historia usiyoipenda ni wajibu wake kimaumbile kukulinda na uwezekano wa kukuathiriwa na hatari hiyo hiyo.
Wengi wetu hupambana kujisahaulisha maumivu kwa kujifanya hatuujui ukweli. Tunaugeuza simulizi. Tunageuza kibao ili kujinasua na hatia, majuto na aibu. Tunachana picha za wapenzi wetu wastaafu tena saa nyingine tukijiapiza kulipiza kisasi. Tunafuta namba za wanaotuudhi na wakati mwingine kuhama mtaa. Tunatumia nguvu kubwa kupambana na vipande vya maisha yetu vyenye simulizi za maumivu. Lakini kadiri tunavyojitahidi kuchana-chana kurasa hizo za aibu ndivyo ubongo unavyozidi kutukumbusha uongo tunaoutumia kujidanganya.
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa pale mtu unapoacha kujidanganya na kuukabili ukweli mchungu, pale unapoanza kukumbuka kile kinachokuumiza, ubongo unakuheshimu na kukusaidia kuachilia maumivu uliyonayo. Kama mzaha fulani hivi lakini huo ndio ukweli kuwa ubongo unakusubiri uwe mkweli kwa nafsi yako uukubali ukweli hata kama unakuumiza na kukufedhehesha.
Sema unavyojisikia. Elezea hisia zako waziwazi bila kificho hata kama kwa kufanya hivyo inakuwa kama unajitonesha kidonda kibichi. Kama huwezi kusema basi jaribu kuandika. Tafuta mahali pa kuuandika uchungu unaokusumbua. Ukiweza kupata maneno sahihi yanayobeba uchungu wako ubongo unaanza kukupumzisha kwa kukutengenezea maelezo yanayohitimisha simulizi hilo linalokuumiza. Shida yetu huwa tunafikiri kukwepa hisia ngumu kunasaidia na tusichojua ni kwamba kadri tunavyokwepa ndivyo tunavyousumbua ubongo kuendelea kuona hatari.
Kwa muhtasari kabisa unapona kwa kurudia rudia kinachokuumiza. Uvae ujasiri kukubali kuwa uliumia. Kiri kuwa ulikosea. Kiri kuwa kuna mtu ulimiuumiza. Kiri kuwa kuna mtu uliharibu maisha yake. Ubongo ukishagundua kumbe umeshakubali maumivu yako unaacha kuyaona kama hatari na kukusaidia kuhariri kumbukumbu husika kwa namna isiyoendelea kukuumiza zaidi. Kwa maana nyingine, kadiri unavyojipa ruhusa ya kuyakabili maumivu yako bila kuyaogopa, unauruhusu ubongo kuboresha kile unachokikumbuka. Husahau kwa kusahau. Unasahau kwa kukumbuka.
Umewahi kusikia hoja za mtu ukaishia kuhoji elimu yake? Unamsikiliza unajiuliza hivi ni kweli huyu haelewi anachozungumza? Hofu huzuia kufikiri. Hofu ni hali ya kujisikia hauko salama wala huru. Ukiangalia mchoro huu unaona, kimaumbile, huwezi kutumia akili zako vizuri kudadisi mambo ikiwa hujisikii salama. Ndio maana ni muhimu ukiwa kiongozi uwekeze vya kutosha kuwafanya watu waamini wako salama ili wasitumie nguvu na muda mwingi kujihami kuliko kufikiri.
Lakini pia, huenda umewahi kujiuliza kwa nini mtu anaweza kutetea kitu anachojua vizuri kabisa kuwa hakina maana. Kwa nini wapenzi hupuuza viashiria vyote vya mienendo wanayokuja kuithibitisha baadae? Jibu lipo hapo hapo kwenye usalama wa kihisia.
Ukishakuwa na maslahi na mtu, kuna kitu unakihitaji kwake, ubongo wako una kawaida ya kukusaidia kutunza usalama wa mahusiano yenu kwa kufikiri kinachoendana na hisia zako—ndio maana kushauri watu waliopendana ni kujichosha.
Christian Bwaya retweeted
naamini moja wapo ya njia inayoweza kukusaida u-treat watu vizuri, kwa heshima, ni kusoma fasihi. hadithi. naamini watu katili na waovu si wasomaji wazuri wa hadithi. umewahi kusikia kwamba 'facts' zinaweza sizibadili mtazamo wa mtu lakini hadithi inaweza? ni kweli, mimi shahidi!
Unapoona mtu mwema anashambuliwa kwa vitu ambavyo hata mtoto mdogo anajua wazi ni uongo, ndio ujue waovu wanajaribu kupambana na hatia wasiyotaka kuikiri.
Christian Bwaya retweeted
Si kila mtu wa jinsia tofauti anayekusogelea huwa ana njaa ya kupendwa kimwili apate utoshelevu wa kimwili. Kuna watu ukitaka kuharibu na kuwachosha endekeza mazungumzo mepesi-mepesi yenye mwelekeo wa kuwatamani kimwili. Hawa, aghalabu, ni watu wenye mahaba makubwa na kujifunza mambo mapya.
Kinachoimarisha ukaribu wenu si msisimko wa kimwili kama ulivyozoea bali msisimko wa kiakili unaotokana na uwezo wa kubadilishana maarifa na uzoefu. Ukiweza kuidodosa misimamo yake na kuchokoza fikra zake kwa staha kwa kuuliza maswali sahihi na kumshirikisha uzoefu bila kumfanya ajione mjinga, mnakuwa marafiki mlioshibana sana. Mahaba yenu yanajengwa kwenye ukuaji wa kiakili.
Hili kwa hakika si kwa urafiki wa kawaida peke yake bali hata uhusiano wa kimapenzi. Kama tulivyoona awali, hata mapenzi hayajengwi na mvuto na utoshelevu wa tamaa za mwili. Ukiwa aina ya mtu unayeweza kusisimua akili ya mpenzi wako na kuichokoza kufikiri tofauti bila kumvunjia heshima unaimarisha ukaribu wenu kwa kiasi kikubwa—kuliko hata mtu anayetumia muda mwingi kujifunza ufundi wa ngono.
Christian Bwaya retweeted
Mahusiano yetu ukubwani, mara nyingi hufukua makaburi ya ugumu tuliokutana nao utotoni. Ukubwani mapenzi yanatuweka kwenye nafasi kubwa ya kukumbuka makovu ya kihisia ambayo wakati mwingine tuliyachukulia kama sehemu ya utoto wetu na hatukupata fursa ya kuyashughulikia. Makovu mengine ni sugu maana ndiyo yaliyotusaidia kuishi na watu waliotupuuza, wasiotuhitaji na kutuumiza.
Usione ni kawaida unapokuwa na kiu ya kumfanya mwenzako awe mtumwa wa matarajio yako. Usione ni kawaida kukinai na kuchoshwa mtu akikupenda, kuona yeye ndiye wa kuupambania uhusiano kwa vile umejitosheleza na huhitaji mahusiano. Usione ni kawaida kukuza makosa ya mwenzako, kujiona uko sahihi muda wote huhitaji kubadilika wala kuomba msamaha.
Mkusanyiko wa kumbukumbu ya kutelekezwa kihisia na watu uliowaamini utotoni, watu uliowaheshimu na kuogopa kuwaumiza, mfano wazazi, ndio ulio nyuma ya ugumu unaoupata leo—kumwamini mtu, kumpenda, kumwelewa, kumpa furaha anayostahili, kumvumilia na kumpa nafasi kujirekebisha anapokukosea. Kwa lugha rahisi matatizo mengi unayokutana nayo kwenye dunia ya mapenzi ukubwani yamechochewa na ugumu wa kihisia uliopitia kama mtoto.
Ukiwa mkweli wa nafsi yako, ukaacha kujidanganya na kufikiri tatizo ni watu wasiokuelewa; ukaacha kujizungushia marafiki wasioweza kukuonesha makovu haya; ukiweza kuuvaa ujasiri wa kujifunza athari za makovu hayo ya utotoni kwenye maisha yako ya kimapenzi, unaweza kabisa kubadili hali ngumu unayokutana nayo kwenye mapenzi mara kwa mara.
Christian Bwaya retweeted
💻 Strengthening digital health systems in Kigoma!
Health centres and dispensaries in Kigoma Region are receiving computer equipment to strengthen the use of GOTHOMIS and Health Management Information Systems (HMIS), supporting improved health data management and reporting at the facility level.
This initiative is part of the UN Kigoma Joint Programme (UNKJP), with support from the Embassy of Ireland, contributing to stronger health information systems and evidence-based decision-making.
#DigitalHealth #HealthInformationSystems #UNKJP #IrelandInTanzania
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya @MayengoDr
Tunaisho kwa ajili yetu zaidi kuliko namna tunaishi kwa ajili ya jamii.
Tunaona kuwa na hospital na shule nzuri karibu sio muhimu, kama kuombwa msaada wa lift na watoto wa shule au mgonjwa 😀