Pinned Tweet
Pumzika kwa Amani Deus mgengele hatutasahau ukatili samia alio fanya juu ya watanzania wazalendo 馃挃馃槶
kuringe sawere Timbiri retweeted
ARBITRARY ARRESTS-UKAMATAJI HOLELA
Neema mhanuzi katibu wa Bawacha mkoa wa kigoma amechukuliwa na watu waliojitambulisha kua ni Askali wa Jeshi la police.
Amechukuliwa Nyumbani eneo la Mwasenga, kata ya Buhanda. Kigoma mjini majira ya SAA 12 Jioni.
Viongozi wa chadema pamoja na familia wamemtafuta vituo vyote vya police mjini kigoma, police wamekanusha kua hawamshikilii wao, ingawa wamesema warudi kesho asubuhi kituo kikuu cha police Mnarani.
Free Neema Mhanuzi now
kuringe sawere Timbiri retweeted
馃毃TAARIFA MBAYA馃毃
Nimefahamishwa na vijana wangu wa mtaani kuwa watu watatu walifika mtaani na kuniulizia na kutaka kujua ninapoishi.
Nikiwa mtu ambaye tayari nimewahi kupitia tukio la utekaji na mateso, siwezi kupuuza taarifa ya aina hii.
kuringe sawere Timbiri retweeted
@tanpol, kama mnanihitaji, nileteeni wito rasmi wa kisheria, nitafika. Sina sababu ya kukwepa sheria, lakini pia sitakubali kuishi kwa vitisho na hofu.
Ninaitaarifu jamii, wanaharakati na taasisi za haki za binadamu kufuatilia taarifa hii. @MariaSTsehai @Sativa255 @AmnestyKenya
馃毃TAARIFA MBAYA馃毃
Nimefahamishwa na vijana wangu wa mtaani kuwa watu watatu walifika mtaani na kuniulizia na kutaka kujua ninapoishi.
Nikiwa mtu ambaye tayari nimewahi kupitia tukio la utekaji na mateso, siwezi kupuuza taarifa ya aina hii.
@tanpol, kama mnanihitaji, nileteeni wito rasmi wa kisheria, nitafika. Sina sababu ya kukwepa sheria, lakini pia sitakubali kuishi kwa vitisho na hofu.
Ninaitaarifu jamii, wanaharakati na taasisi za haki za binadamu kufuatilia taarifa hii. @MariaSTsehai @Sativa255 @AmnestyKenya
kuringe sawere Timbiri retweeted
Leo Media zote kubwa huko Duniani mjadala ni Hukumu ya Mhe. Lissu.
Kazi nzuri wakili msomi @TitoMagoti
kuringe sawere Timbiri retweeted
Tanzania High Court's ruling acquitting comrade Tundu Lissu of the politically motivated treason charges is a victory against the ultimate weapon of state intimidation. The Tanzanian regime tried to threaten him with the death penalty simply for demanding free, fair, and transparent electoral reforms but failed to prove its malicious claims because truth cannot be hidden by judicial overreach.
However, the decision to convict him on the engineered, lesser charge of "incitement" and to sentence him to four years in prison is a glaring reminder of how autocrats weaponize the judiciary to silence legitimate opposition. Convicting him for his rightful defense of democracy - his call for "No Reforms, No Election" - proves that the state manufactured an offense purely to keep a powerful voice of the people locked away.
From Kampala to Dar es Salaam, our struggle against generational dictatorships and electoral autocracy remains unified. A cage can restrain bodies, but it can never imprison the spirit of freedom ignited across the region.
We stand with you, Chadema, and with you the great people of Tanzania, in rejecting the ongoing persecution. Aluta Continua!
kuringe sawere Timbiri retweeted
Leo Media zote kubwa huko Duniani mjadala ni Hukumu ya Mhe. Lissu.
Cc. @TitoMagoti
kuringe sawere Timbiri retweeted
Mh Lissu anahukumiwa MIAKA MINNE JELA.
Yote yaliyosemwa yametimia. Dunia nzima imeona na imesikia.馃挃馃挃馃槶馃槶
#FreeTunduLissuNow
Mh Lissu anahukumiwa MIAKA MINNE JELA.
Yote yaliyosemwa yametimia. Dunia nzima imeona na imesikia.馃挃馃挃馃槶馃槶
#FreeTunduLissuNow
kuringe sawere Timbiri retweeted
We want Lissu granted his freedom!
The judges were not listening to a case of sedition but TREASON - he has been acquitted!
What is going on is MENTAL ACROBATICS to please Samia Suluhu who is sh*t scared of Lissu!
#FreeTunduLissu nothing more or less
kuringe sawere Timbiri retweeted
Kupitia yanayoendelea Mahakamani leo, bado kuna watu wanaowabeza na kuwadharau wanaharakati hawa?
Kama mlidhani walikuwa wanapiga kelele bila sababu, sasa ni wakati wa kutafakari.
Ombeni msamaha kwao. Wakati mwingine ukweli huchelewa kueleweka, lakini hauwezi kufichwa milele.
Kupitia yanayoendelea Mahakamani leo, bado kuna watu wanaowabeza na kuwadharau wanaharakati hawa?
Kama mlidhani walikuwa wanapiga kelele bila sababu, sasa ni wakati wa kutafakari.
Ombeni msamaha kwao. Wakati mwingine ukweli huchelewa kueleweka, lakini hauwezi kufichwa milele.
kuringe sawere Timbiri retweeted
Tumshukuru Mungu sana kwa maisha ya Tundu Lissu. Mwaka na miezi nane iliyopita umekuwa wa kujitoa mhanga kwa ajili ya nchi yetu. What a Man!!
kuringe sawere Timbiri retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 500
Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini.
Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning鈥檌ng鈥檌nia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini????
Maana yake ni nini waheshimiwa majaji?
Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini.
Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo.
Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji.
Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu,
Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili.
Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza.
Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham.
Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.
Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.















