#NiYeye retweeted
Mtoto wa Mkulima ukiwa unajitafuta achana na kitu kinaitwa “interest,Ndoto yangu” Jipate kwanza hayo mengine utayafanya tu Piga kila kazi.
Good morning Champ
#NiYeye retweeted
Mwenyekiti wetu Tundu Lissu amezishinda risasi 32 za ccm na dola..
Walitaka kumuua mwaka 2017 wakashindwa.
Wamejaribu kumnyonga kwa kesi ya uhaini wa uongo wameshindwa.
Wamemfunga kwa uchochezi wa uongo.
Makaburu hawakuwahi kumpiga risasi Mandela wala kumuondolea ubunge wake.
Wamlimfunga tu kwa mda mrefu na baadae alitoka.
Historia ya Mwenyekiti Lissu itaandikwa kwa wino wa dhahabu, sio Raila wala Mandela amefanyiwa unyama na serikali kama ambao Mwenyekiti Lissu amefanyiwa na anaendelea kufanyiwa.
Tutashinda na tutavuka.
#NiYeye retweeted
BABYLON SYSTEM IS THE VAMPIRE!
Hii ni TAARIFA YA DHAMIRA YA KUKATA RUFAA (NOTICE OF INTENTION TO APPEAL) iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Tanzania katika Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) Tanzania.
Kwa lugha rahisi, kupitia hati hii DPP anaonyesha kwamba hakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu kesi ya Tundu Antiphas Lissu, na anataka kupinga uamuzi huo katika Mahakama ya Rufani.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ndiye anayeleta rufaa. Tundu Antiphas Mughwai Lissu ndiye anayekatiwa rufaa, katika Mahakama ya Rufani. Hati hiyo imewasilishwa tarehe 13 Novemba 2026.
Kwa mujibu wa hati hii, tarehe 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam ilitoa uamuzi katika Kesi ya Jinai Na. 19605 ya mwaka 2025, Jamhuri v. Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
Mahakama Kuu ya Tanzania Ilimuachia huru Tundu A.M Lissu katika shtaka la uhaini (Treason) na ilimkuta na hatia ya kuchochea kutendeka kwa kosa la jinai (Inciting the Commission of an Offence)
Mahakama ilitoa hukumu kwa Tundu A.M Lissu kifungo cha miaka minne gerezani. DPP ameeleza hakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru TAL katika shtaka la uhaini.
Hivyo, DPP anataka Mahakama ya Rufani Tanzania ichunguze upya uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kumuachia huru Tundu Antiphas Mughwai Lissu katika shtaka hilo la uhaini.
DPP hajaonyesha anakata rufaa dhidi ya hukumu ya kifungo cha miaka minne. Hati inaeleza rufaa inahusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika shtaka la uhaini na amri ya kumuachia huru Tundu Lissu.
DPP ameomba Mahakama impatie nakala ya hukumu na kumbukumbu za mwenendo wa kesi (Judgment and Proceedings) haraka iwezekanavyo ili aweze kuendelea na mchakato wa kukata hiyo rufaa.
DPP anataka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru Tundu Lissu katika shtaka la uhaini. Anataka Mahakama ya Rufani ipitie ushahidi na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu.
Kwa kifupi, DPP anasema;
“Jamhuri hatujaridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru Tundu Antiphas Lissu katika shtaka la uhaini. Tunakusudia kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ili uamuzi upitiwe upya”
Hii ni taarifa ya nia ya kukata rufaa, si hoja zote za kisheria za rufaa (Grounds of Appeal). Haijafahamika ni hoja gani ambazo DPP anataka kuzitumia kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
NB; Hawa viumbe ndiyo wanaotaka tukae chini na kuzungumza? Tazama sasa matendo yao. Hawana nia njema hata kidogo, na hawawezi kubadilika. Ni watu wa hila, wadanganyifu, na wasioaminika.
#NiYeye retweeted
Kesho kuna mambo haya ✌🏾
Kutakuwa na uzinduzi rasmi wa Makao Makuu ya Kuratibu AFCON 2027 jijini Dar es Salaam, pamoja na utiaji saini rasmi wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Hii COMBINATION ya Lissu na @HecheJohn haijapata kuwepo kwenye UONGOZI wa aina yoyote hapa nchini. Najaribu kufikiria kama Lema au Wenje ndie angechaguliwa kuwa Makamu saa hizi CHADEMA ingekuwa wapi? Mungu ni Mwema kila wakati.
#NiYeye retweeted
WATU WALIOKUWA NA MAJIBU YA KUSHANGAZA MBELE ZA MUNGU KWENYE BIBLIA 😂
1. KAINI – MWANZO 4:9
Mungu alimuuliza: “Habili ndugu yako yuko wapi?”
Kaini akajibu: “Sijui; mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” 😂
2. YONA – YONA 4:9
Mungu akamuuliza: “Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango?”
Yona akajibu: “Ninatenda vema kukasirika hata kufa!” 😂
3. GIDEONI – WAAMUZI 6:13
Malaika wa Bwana akamwambia: “Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.”
Gideoni akajibu: “Ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata?”
4. HABAKUKI – HABAKUKI 1:2
Habakuki akamuuliza Mungu: “Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia?”
Akaendelea kulalamika kuhusu uonevu na ukosefu wa haki
5. DAUDI – ZABURI 13:1
Daudi akamuuliza Mungu: “Ee Bwana, hata lini utanisahau daima? Hata lini utanificha uso wako?”
6. AYUBU – AYUBU 30:20
Ayubu akamwambia Mungu: “Nakulia wewe, lakini huniitikii; nasimama, nawe hunijali.”
7. YEREMIA – YEREMIA 20:7
Yeremia akamwambia Mungu: “Ee Bwana, umenishawishi, nami nikashawishika.”
Akaendelea kueleza jinsi alivyokuwa akidhihakiwa na kuchekwa kila siku
8. MUSA – HESABU 11:11–12
Mungu alipompa jukumu la kuwaongoza Waisraeli, Musa akamuuliza kwa nini amemletea mtumishi wake shida hiyo na kwa nini amewekewa mzigo wa watu wote hao
9. ELIYA – 1 WAFALME 19:4
Akiwa amechoka na kukata tamaa, Eliya alimwambia Mungu: “Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu.”
10. ZEKARIA – LUKA 1:18
Malaika Gabrieli alipomwambia kuwa atapata mtoto, Zekaria akajibu: “Nitajuaje neno hili? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mzee sana.”
11. SARA – MWANZO 18:12–15
Mungu alipomuuliza Sara kwa nini amecheka baada ya kusikia ahadi ya kupata mtoto, Sara akajibu: “Sikucheka.”
Mungu akamwambia: “La, umecheka.”
12. ABRAHAMU – MWANZO 18:23–25
Abrahamu alipokuwa akizungumza na Mungu kuhusu Sodoma, akamwuliza: “Je! Utamwangamiza mwenye haki pamoja na muovu?”
Akaendelea kujadiliana na Mungu kuhusu idadi ya wenye haki ambao wangeweza kuokoa mji
Biblia ina watu wenye maswali, malalamiko, ujasiri na majibu ya kila aina
#NiYeye retweeted
Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Badala yake, chagua lishe bora yenye virutubisho muhimu kwa afya njema.
#TransFatFreeTz
#TransFatFreeEAC
@TawlaTZ
#NiYeye retweeted
Shauri la kisheria kuhusu ubingwa wa AFCON 2025 lililofikishwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) linatarajiwa kupata uamuzi wake kesho, Jumanne Novemba 24, 2026 majira ya mchana, kutoka makao makuu ya CAS, Lausanne, Uswisi
Uamuzi huo utaamua hatma ya ubingwa kati ya Morocco na Senegal, ambapo upande utakaoshinda rufaa hiyo utakuwa na haki ya kutambuliwa kama bingwa wa AFCON 2025
Senegal inapinga uamuzi wa CAF ulioipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3–0 licha ya Senegal kushinda uwanjani kwa bao 1–0
All eyes on Lausanne. Who will be crowned Africa’s champions? Nanini maoni yako?
#NiYeye retweeted
Replying to @Mwinshehe07
Kila mwenye kusubiri yupo pamoja na mwenyeziMungu
Na hili nimelithibitisha kama ni kweli
#NiYeye retweeted
Kabla haujazima data naomba niandikie mstari mmoja kwenye Biblia au Qur’an ambao unakutia nguvu
#NiYeye retweeted
Replying to @Mwinshehe07
Mwanzo 28:15
Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
#NiYeye retweeted
Replying to @anuskills3
Wewe unaamini ukiwa CCM ndio unasifia kila kitu? Kenya imetupita kwenye maeneo mengi na hizi ni facts za World Bank na taasisi nyingine
• GDP 2025: Kenya USD bilioni 135.94 wakati Tanzania tuna USD bilioni 90.14 tofauti ya USD billion 45.8
• GDP per capita: Kenya USD 2,362.9 sisi Tanzania tuna USD 1,318.8
• Upatikanaji wa umeme 2024: Kenya 77% wakati Tanzania 52.4%
• Matumizi ya intaneti 2024: Kenya 35% sisi Tanzania 31%
• Umeme unaozalishwa kwa renewable sources 2024: Kenya 91% wakati Tanzania tuna 52%
• Financial inclusion: 84.8% ya watu wazima Kenya wanapata huduma rasmi za kifedha wakati sisi Tanzania 59.8%
• Startup ecosystem: Kenya ilivutia USD milioni 984 za uwekezaji kwenye startups mwaka 2025 karibu theluthi moja ya uwekezaji wote wa startups Afrika Tanzania tulikuwa na USD million 20
* Nairobi ni kitovu muhimu cha fintech na teknolojia Afrika
* Kenya ina Lake Turkana Wind Power mojawapo ya miradi mikubwa ya upepo Afrika
* Inaongoza kikanda kwenye ubunifu wa huduma za fedha kupitia M-Pesa
* Ina nafasi muhimu ya usafiri wa anga kupitia JKIA na Kenya Airways


























