Bwibwi retweeted
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. ”
Yos 1:8 SUV
Bwibwi retweeted
JITAHIDI sana usiwe chanzo cha kupotea kwa rizki ya mtu yeyote. Tunakutana kwenye hustle huko hatujuani ila wengi wetu majumbani tumeacha “timu ya mpira” inayotusubiri jioni turudi na kitu mkononi. Tufanyiane yote sisi kwa sisi lakini mirija yetu ya rizki isuguswe please 🙏🏿
Bwibwi retweeted
Tunashukuru si kwa sababu maisha hayana changamoto, bali kwa sababu hata katikati ya changamoto, tumekuwa na sababu za kutambua wema, rehema, ulinzi na uaminifu wa Mungu.🙏🏼
Bwibwi retweeted
Tumshukuru mwenyezi Mungu, mwingi wa upendo na upaji, kwa kutupatia tena uhai asubuhi ya leo
Nakutakia Jumatatu njema uwe na wiki ya furaha na mafanikio
Bwibwi retweeted
Leo usikubaliane na hali ya kukata tamaa.
Omba, inuka, anza kwa hatua ndogo na endelea kusonga mbele.
Kuna siku zinaanza slow, zinachangamka later, SHOW UP 🤛🏼
Bwibwi retweeted
Maisha yanaweza kuleta Dhoruba zisizotarajiwa, lakini una Mungu Mwaminifu ambaye hatakuacha kamwe, wakati kesho inapoonekana kutisha, kumbuka kuwa Maisha yako ya baadae yako salama mikononi Mwake, endelea kumwamini na kusonga mbele,
Bwibwi retweeted
Mungu baba uwaepushie magonjwa makubwa yatakayoathiri uchumi wetu wale wote wanaotutegemea🤲🏾🙏🏾
Bwibwi retweeted
Mabadiliko makubwa ya maisha yako ya baadae ni matokeo ya maamuzi madogo madogo unayo yafanya kila ziku
Bwibwi retweeted
Kukubali kuwa unaweza kujiboresha na kuwa kile unachotaka,bila hofu ,ni uwezo wajuu wa akili.
Bwibwi retweeted
Kuna jambo nililitaka mie kwa kina haswa lakini nikalikosa kwa namna ya ajabu tu kwa kweli.
Mungu akanipa jengine lenye utendaji tofauti lakini hitimisho the same.
Kusema la ukweli, lile la Mungu limekuwa bora sana kimatokeo kuliko nilivyokadiria.
Mungu ni mkubwa always.
Umewahi kukutana na watalaka washikaji? Hawa ni watu wameachana kwa talaka, tena mahakamani, lakini wanaishi maisha yasiyo na ugomvi wa wazi na kama ulikuwa unawajua wote wawili huwezi hata kuhisi walishaachana.
Ndio nilichokutana nacho leo asubuhi. Tunasafiri leo asubuhi halafu mtalaka kamleta mtalaka wake mahali pa kuanzia safari. Wamesaidiana mabegi, wakaagana kwa kumbatio, kisha mtalaka karudi na gari la mtalaka wake kulirudisha nyumbani kwa mtalaka wake. Namwuuliza huyu mtalaka ninayesafiri naye wamewezaje ‘kuachana bila kuachana’?
“Mtu anaweza kushindwa kuwa mume mzuri kwako lakini akaweza kabisa kuwa baba mzuri wa watoto wenu. Mtu mwema kabisa anaweza kushindwa kuendana na wewe kama mpenzi lakini akabaki kuwa rafiki mzuri ukimuelewa. Hapo anaenda kwa watoto wake (hawajui tuna miaka miwili ya talaka) na kesho kutwa anarudi kazini kwake.”
Imenichoma maana sijazoea. Kwa wengi wetu, ukishashindwa kuwa mpenzi wangu maana yake huwezi tena kuwa mama na kamwe hatuwezi tena kuwa marafiki. Unadhani hii inachangiwa na nini? Kwa nini ukishashindwana na mtu aliyewahi kuwa mpenzi wako, lazima muendeleze ugomvi, visasi, vitimbi na hata uadui? Kwa nini tunafikiri mtu akikushindwa wewe kama mpenzi wake (mstaafu) basi lazima ashindwane na watoto wenu, ndugu zenu na hata marafiki mliwahi kuchangia?
Bwibwi retweeted
Kama unataka kujifunza, tenga muda wa kujifunza.
Kama unataka kuweka akiba, tenga pesa kabla ya matumizi yasiyo ya lazima.
Kama unataka kuwa na biashara, jifunze kuhusu wateja, bidhaa na masoko.
Kama unataka kuwa na afya bora, jali mwili wako.
Usisubiri uwe na hamasa. Anza na kile ulicho nacho.
Bwibwi retweeted
Siku moja, Mungu ana matumizi nayo balaa.
It can change everything.
Keep grinding, keep your hopes.
Bwibwi retweeted
Kanisani tunahubiriwa kuwa watu wema; watu wa haki; watu wa upendo; na watu wa kuwajali wengine. Sijui nini huwa kinatupata mara tu baada ya kutoka nje ya nyumba za ibada 🤔




















