Sucha (@Sucha2073) profile picture
Joined May 2024
Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)Photo by Sucha (@Sucha2073)
Kuna mtu nilikutana naye ambaye hajawahi kuweka picha ya mafanikio yake kwenye mitandao ya kijamii Ana nyumba, magari na biashara, lakini hata watu wanaomfaham hawajui maisha anayoishi Nilimuuliza kwa nini anaficha mafanikio yake. Jibu lake lilikuwa tofauti kabisa na nilivyo....
5
36
2
407
36,053
1.Urithi wa mfumo dume katika jamii Jamii nyingi zimejengwa katika mfumo ambao mwanaume ndiye kichwa cha familia, mwenye mamlaka ya mwisho na mtoa maamuzi makubwa. Hapa mwan'ke ndiye anayetarajiwa kurekebisha tabia zake ili familia iendelee kuwa na utulivu na amani Rejea biblia.
Tuna mafundisho mengi ya ndoa yanayoelekeza wajibu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Walimu wengi wa ndoa, kwa mfano, wanafikiri mwanamke akiwa mtii, akajua kumhudumia mwanaume na namna ya kuongea naye kwa unyenyekevu, basi matatizo mengine ya ndoa yataisha. Unafikiri ni kwa nini? Kwa nini walimu wa ndoa hutumia lugha yenye jinsia inayoonesha kuwa tatizo kubwa kwenye mahusiano ni mwanamke? “Mwanaume anataka utulivu.” “Mume hataki kelele.” “Mwanaume hataki uchafu.” “Mume anataka kuwa sauti ya mwisho.” “Mwanaume hatari kuambiwa cha kufanya.” Kwa nini tunafikiri matatizo mengi ya kitabia tunayoyaona kwa mwanaume husababishwa na mwanamke? Kwa nini walimu wengi hawazungumzi na wanaume moja kwa moja na wanafikiri mwanaume akiwa na udhaifu fulani basi lawama zielekezwe nyumbani kwake kwa mke wake—na kwamba mwanamke akibadilika tatizo linaisha? Walimu wachache wanaozungumzia ‘Side B’ wanaongelea zaidi tendo la ndoa. Kwamba wanaume akiwa na nguvu za kiume, akala ugali maharage akashiba, halafu akawa na hela za kuhakikisha mke wake amependeza, shughuli yake imeishia hapo. Msingi hasa wa mawazo haya ni nini? Je, ni kweli anachokihitaji zaidi mwanamke kwa mume wake ni mume mwenye nguvu za kiume na uwezo wa kipesa na kwamba mengine yote yanarudi kwenye utii na unyenyekevu kwa mumewe?
3
31
Kwahiyo ukiangalia kwamba mwanaume ni mtu ambaye mahitaji yake ya kihisia yanapaswa kulindwa, lakini mwanamke ndiye anayepaswa kuyatimiza. Hoja ya kwanza ni urithi wa mfumo dume
6
Lakin embu angalia Wakolosai 3:19: "Enyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu nao."
8
Waefeso 5:22–24 "22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo"
10
Sucha retweeted
Tuna mafundisho mengi ya ndoa yanayoelekeza wajibu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Walimu wengi wa ndoa, kwa mfano, wanafikiri mwanamke akiwa mtii, akajua kumhudumia mwanaume na namna ya kuongea naye kwa unyenyekevu, basi matatizo mengine ya ndoa yataisha. Unafikiri ni kwa nini? Kwa nini walimu wa ndoa hutumia lugha yenye jinsia inayoonesha kuwa tatizo kubwa kwenye mahusiano ni mwanamke? “Mwanaume anataka utulivu.” “Mume hataki kelele.” “Mwanaume hataki uchafu.” “Mume anataka kuwa sauti ya mwisho.” “Mwanaume hatari kuambiwa cha kufanya.” Kwa nini tunafikiri matatizo mengi ya kitabia tunayoyaona kwa mwanaume husababishwa na mwanamke? Kwa nini walimu wengi hawazungumzi na wanaume moja kwa moja na wanafikiri mwanaume akiwa na udhaifu fulani basi lawama zielekezwe nyumbani kwake kwa mke wake—na kwamba mwanamke akibadilika tatizo linaisha? Walimu wachache wanaozungumzia ‘Side B’ wanaongelea zaidi tendo la ndoa. Kwamba wanaume akiwa na nguvu za kiume, akala ugali maharage akashiba, halafu akawa na hela za kuhakikisha mke wake amependeza, shughuli yake imeishia hapo. Msingi hasa wa mawazo haya ni nini? Je, ni kweli anachokihitaji zaidi mwanamke kwa mume wake ni mume mwenye nguvu za kiume na uwezo wa kipesa na kwamba mengine yote yanarudi kwenye utii na unyenyekevu kwa mumewe?
12
17
3
39
2,445
Sucha retweeted
Hakuna anayekuja kukuokoa. Hakuna. Kila mtu anapambana na mambo yake. Ukisubiri msaada utawalaumu wengi ambao nao wana shida zao wasizoweza kukuambia.
3
31
62
1,550
mnyika asimamie kanuni za nidhamu za chama, na chadema isivumilie wanaopingana na maamuzi rasmi ya chama, tena waziwazi. mtachanganya w’nchi. chama kimeweka msimamo wake hadharani kuhusu kinachoitwa maridhiano, kujitokeza na kusema tofauti ni kiwango cha juu cha kukosa adabu!
19
128
7
600
24,939
Binadamu hahitaji tu kuishi, anahitaji kuhisi kwamb maisha yk yana sbb na yana maana. Mtu anaweza kuwa na pes, nyumba nzuri, chakula na huduma bora, lkn akahisi maisha yake hyn maana. Mwingine anaweza kuwa na maisha magumu sana, lkn bad akawa na kt kinachomfany aamke kila asubuh
Umewahi kujiuliza kitu gani hasa huweza kumpa nguvu mtu anayepitia mateso? Kwa nini wengine wakipitia uonevu kidogo nyuso zinafubaa, miili inadhoofu, wanapata sonona, na wakati mwingine wanajihukumu kwa kujitoa uhai? Kwa nini kuna mtu anaweza kuumizwa vikali na bado unamwona ananawiri, uso wake haukosi nuru, anatabasamu na wakati mwingine yeye ndiye anayewatia moyo nyie mnaomhurumia? Viktor E. Frankl aliandika kitabu hiki miongo kadhaa iliyopita. Man’s Search for Meaning—Kuisaka ‘maana’ ni mojawapo ya vitabu bora tunavyovitumia kufundishia unasihi. Kitabu kinasimulia mateso na ukatili wa kutisha kwenye kambi tatu za utesaji zilizoendeshwa na ma-Nazi mara tu baada ya vita kuu ya pili ya dunia: 1) Auschwitz (Poland), 2) Theresienstadt (Czechoslovakia) na 3) Kaufering (Ujerumani) Sehemu ya kwanza ya kitabu ni ngumu hata kusoma. Unajiuliza binadamu anawezaje kuwa mkatili kwa kiwango hiki? Frankl, kwa mfano, anaeleza namna walivyofanyishwa kazi ngumu katika mazingira yenye baridi kali. Kinachotisha zaidi ni namna Manazi walivyowaua. Fikiria mmeteseka na kazi ngumu, mnashindia uji, halafu mnapangwa kwenye mstari na anayeonekana amedhoofu aliuawa. Fikiria maisha hayo ya kutokujua kesho itakuwaje maana zamu yako ya kufa ni dakika yoyote. Kuna sehemu za kitabu hiki, kusema ukweli, nikiri nilishindwa hata kuzisoma. Frankl aligundua kwamba hata katika hali mbaya kiasi hicho, wapo binadamu walibaki kuwa majasiri. Humo kambini Frankl aliona tofauti kubwa kati ya wale waliokata tamaa na wale waliobaki na ujasiri wa kukikabili kifo wasichojua kitawafika lini. Hapa ndipo ilipo nadharia yenyewe. Kwamba wale waliovumilia kuteseka mara nyingi walikuwa watu wanaoona zaidi ya mateso wanayopitia—labda ile imani kuwa ipo siku wangeonana na familia zao, labda tumaini kuwa siku moja wataishi kuzisaidia jamii zao, au ile nguvu ya dhamira kwamba ukweli na haki hatimaye vingeshinda hata kama wenyewe wangekufa. Frankl anasema kuona zaidi ya mateso ndio ‘maana’ yenyewe na ukishaipata ‘maana’ mateso unayopitia hayawi na nguvu yoyote. Tukirudi kwenye aya ya kwanza, kukata tamaa na kuchoka inaweza rahisi ikiwa mtu hajui kwa nini anateseka. Watu wanaozujua ‘maana’ zao huwa wana nguvu ya kukubali kupitia njia ya moto ili kile wanachokiona kitokee. Hawa ndio wale watu ambao unaweza kuwahurumia na kuwalilia na wao wenyewe wakakufariji. Nikuache na swali: Kipi hasa kinakuchochea kufanya chochote unachokifanya? Unaishi ili uifanyie nini jamii yako? Usipolijibu swali hili pesa, mali, starehe, madaraka vitakuwa vya maana sana kwako na mateso kidogo tu yanatosha kukutikisa na kukufanya uusaliti utu wako na chochote ulichowahi kukipigania. Frankl anatukumbusha kuwa utoshelevu katika maisha hauletwi na hivi vitu tunavyoviona—mali, starehe, elimu, madaraka, nguvu bali kuipata ‘maana’ na kuipigania.
1
1
111
Kwa mfano, mtu anaweza kupata maana kupitia familia yake, mwingine kupitia dini, mwingine kupitia kazi yake, na mwingine kupitia kusaidia watu wasiojiweza.
14

40
2,123
Congratulations, Dr. Moses Maka Ndimukika🎉 A new chapter of leadership and service begins. May God grant you wisdom to lead, courage to make a difference, and grace to shepherd His Church faithfully. May your leadership advance God’s mission across the East-Central Africa Division. Wishing you a fruitful and blessed tenure🙏🏽
6
1
27
677
The Adventist Church has elected Moses Ndimukika Maka as East-Central Africa Division president and Tom Ogal as executive secretary. Both assume their roles immediately. #ANN #AdventistNews Read more. adventist.news/news/new-lead…
2
22
3
134
2,992
The General Conference Executive Committee of the Seventh-day Adventist Church voted on November 2, 2026, to approve Dr. Moses Ndimukika Maka as the next president of the East-Central Africa Division and Dr. Tom Ogal as Executive Secretary.
3
31
1
145
2,774
Rest well Heroes
7
40
1
145
2,063
Zab 41:1 (SUV) Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu.
46
150
10,216
Today, the U.S. Embassy community joined me to honor the memory of all those who lost their lives in the violence surrounding Tanzania’s October 2025 general elections. We remember them, and the families who still grieve and seek answers. As I said to the U.S. Senate during my confirmation hearing, this will not be swept under the rug.
237
1,258
63
3,378
111,298
Sucha retweeted
Ukiweza kutofautisha hisia za ngono na mapenzi uwezekano wa mahusiano unayoyaanzisha kudumu unakuwa mkubwa. Hisia za ngono, tamaa, ni msukumo wa kimwili unaowachochea wanyama kuzaliana. Nzi, pamoja na udogo wake anazo hisia hizi—sexual instincts—ingawa hana mapenzi. Hisia za ngono (tamaa) zikiwa kipaumbele chako, vigumu kuwekeza kwenye mahusiano yanayokutanisha fikra na kuruhusu mikinzano ya mawazo kujenga utambulisho wa pamoja—intimacy. Ukaribu wako na mtu, aghalabu, utalenga kukutanisha miili kuliko fikra, imani na mambo yanayowatambulisha (identities). Utavutiwa na mwonekano, utamtamani, ukifanikiwa kukidhi tamaa za mwili hisia hizo zitapoa. Usipozimudu hisia hizi, kama ilivyo kwa nzi, unaweza kucheza na wengi kwa mpigo—maana huwapendi. Mapenzi, tofauti na hisia za ngono, ndizo zinatutofautisha na wanyama wengine. Ukimpenda mtu unahamia kwenye fikra, imani na misimamo yenu. Upendo unakuchochea kuweka mazingira ya kumwamini, kumfanya kuwa sehemu ya faragha yako, na hivyo unampandisha ngazi ya kumruhusu kukufahamu, kuyafahamu matumaini yako, kuzijua aibu zako. Upendo unakuchochea kujitoa ili kumheshimu, kumstahi na kumfanya kuwa sehemu ya maisha yako. Ukaribu wa kiwango hiki ndio unaochochea muunganiko wa utambulisho wenu (identity) ili kuufanya kuwa mmoja. Huo ndio upendo unaodumu, kwa mujibu wa mshunuzi Sternberg. Ingawa uwezo huu anao mwanadamu, ukishakosa upendo wa mzazi utotoni, inaweza kukuwia vigumu mno kumpenda mtu mwingine au hata kumruhusu mtu mwingine akupende kwa kiwango hiki. Katika mazingira kama haya, watu wengi huishia kwenye hisia za ngono, na uwezekano wa ajali nyingi za mahusiano unakuwa mkubwa zaidi. Mchoro: Akili Ige (AI)
1
17
23
1,163
Sucha retweeted
Mapenzi yana tabia ya kukusogeza karibu na mtu kiasi cha kukufumbua macho uuone upande wake mwingine ambao si wengi wamewahi kuufikiria. Kwa kawaida, unapompenda mtu, unalazimika kujifunua na kumruhusu kuuona utoto wako, kuiona historia ya tabia zako, aibu zako, maumivu unayojiuguza, hofu usizozikiri kwa watu, hatia za makosa mengi uliyowahi kuyafanya na hata mazimwi unayojaribu kuyadhibiti yasiharibu taswira yako mbele za kadamnasi. Unapoanza mahusiano na mtu, unakutana na sura nzuri ambayo aghalabu huonekana na wengi wetu—busara, hekima, matumaini, furaha, ujasiri, uzuri wa sura na mengine mengi yanayokufanya umpende. Hata hivyo, kadri kina cha kuaminiana kwenu kinavyoongezeka ndivyo unavyopata ruhusa ya kukutana na tabia za faragha zisizofahamika na wengi. Hapa ndipo unapokutana na ile tofauti ya matarajio na kivuli kinene cha uhalisia wa mtu, hali inayoweza kuzalisha ugomvi mkubwa ambao kimsingi ni mtihani wa kukipokea kivuli cha tabia za mtu kisichoruhusiwa kukutana na watu. Ukiweza kupata mtu anayetambua kuwa mapenzi ni pamoja na kuelewa kuwa wewe ni ‘mradi wa ujenzi’ unaoendelea kushughulikia kivuli chako ambacho wakati mwingine wewe mwenyewe hukitambui; ukimpata mtu anayeelewa kuwa tabia hizo hizo zinazomkera huenda ndizo hizo hizo zilizowahi kukusaidia kukabiliana na utoto wenye upweke, unyonge na maumivu ya kukataliwa na watu uliowahitaji, na kwamba mkidhamiria mnaweza kusaidiana kukua pamoja bila kuzodoana, kuumizana na kulaumiana na hata pale kazi hiyo inapokuwa ngumu visasi na chuki havichukui nafasi, utakuwa mmoja wa watu wanaoishi maisha yenye uhuru na amani.
6
23
61
2,290
Sucha retweeted
“Kama huwezi kuwa na furaha ukiwa peke yako, huwezi kuipata ukiwa na mtu mwingine. Omba omba wawili hawawezi kusaidiana zaidi ya kuongezeana majanga.” —Osho
6
35
2
108
3,744