Tanganyika.Colony retweeted
Huu ujasiri wa kuuona ukatili wote unaofanywa na dola ya Tanzania kama “siasa” mnautoa wapi wazee?
Hivi kweli kinachofanywa na watawala wa Tanzania ni siasa?
Siasa za kuua maelfu ya watanzania wenzako wasiokuwa hatia pasipo tone lolote la hofu?
Siasa za kuteka, kupoteza watu, kupakazia watu kesi za uhaini na kuwasweka jela indefinitely, etc.?
Hii tafsiri ya “siasa” inayotumika hapa ambayo inapaswa kutenganishwa na “uanaharakati” ni ipi hiyo wakuu?
#TajiriLaKihaya
CHADEMA lazima tujifunze kutofautisha UANAHARAKATI na SIASA.
Tukifika mahali tunawaacha wanaharakati watupangie chama chetu kifanye nini, nani awe kiongozi, chama kisimame wapi na kiamue mambo gani, tutakuwa tunakipeleka chama kwenye hatari ya kukiua kwa mikono yetu wenyewe.
Mwanaharakati na mwanasiasa wanaweza kuwa na malengo yanayofanana, lakini majukumu yao si lazima yawe sawa.
Mwanasiasa anawajibika kwa chama, wanachama, sera, wapiga kura na taasisi za chama. Anaingia kwenye uchaguzi, anatafuta ridhaa ya wananchi na anapaswa kufanya maamuzi yanayoweza kubeba chama kizima.
Mwanaharakati, kwa upande mwingine, anaweza kuingia na kutoka kwenye ajenda mbalimbali bila kuwa na wajibu wa moja kwa moja kwa taasisi ya chama. Leo anaweza kuunga mkono CHADEMA kwa sababu anaona chama kinasimamia jambo analoamini; kesho anaweza kukosoa CHADEMA au kuunga mkono nguvu nyingine ikiwa anaona ajenda yake inahitaji kufanya hivyo.
Na hilo si kosa. Huo ndiyo uanaharakati.
Tatizo linaanza pale chama kinapoacha kujenga msimamo wake wa ndani na kuanza kuongozwa na presha kutoka nje.
CHADEMA ni taasisi ya kisiasa. Ina wanachama, katiba, viongozi, vikao, sera na wajibu kwa mamilioni ya Watanzania. Hivyo, maamuzi yake makubwa lazima yatokane na wanachama na mifumo halali ya chama, si kelele za mitandaoni au presha ya watu ambao hawabebi mzigo wa taasisi hiyo.
Na tuwe wa kweli,anayekukosoa si lazima awe adui yako, na anayekusifia si lazima awe rafiki yako.
Wanaharakati wana nafasi muhimu sana katika demokrasia. Wanaweza kuibua matatizo, kuhoji mamlaka, kutetea haki na kusukuma mijadala ambayo wanasiasa wakati mwingine wanaogopa kuigusa. Chama makini kinapaswa kuwasikiliza.
Lakini kuwasikiliza si sawa na kuongozwa nao.
CHADEMA inapaswa kuwa na uwezo wa kuchukua hoja nzuri kutoka kwa wanaharakati, kuzipima kwa sera na misingi ya chama, kisha kufanya uamuzi unaolinda maslahi mapana ya Watanzania.
Pia tunapaswa kuwa waangalifu na ushawishi wa nje. Dunia ya leo ina nguvu kubwa za kiuchumi, kisiasa na kiitikadi zinazojaribu kuathiri mijadala katika nchi mbalimbali. Hii si sababu ya kumshuku kila mwanaharakati kuwa anatumiwa na mtu fulani,lakini ni sababu ya chama kuwa na uwezo wa kuchambua kila ajenda na kujiuliza: Nani anafaidika? Ajenda hii inamlinda nani? Inaendana na misingi yetu? Na mwisho wake ni nini kwa Tanzania?
Hatupaswi pia kuingia kwenye siasa za kuamini kwamba kila anayekuja na fedha, taasisi, NGO au ajenda kutoka nje ana nia mbaya. Lakini vivyo hivyo, hatupaswi kuwa wajinga kiasi cha kuamini kwamba kila ushawishi wa nje hauna maslahi nyuma yake.
CHADEMA inahitaji uhuru wa kimkakati.
Tusijenge chama kinachotegemea personalities za mitandaoni, influencers au wanaharakati maarufu. Watu huja na kuondoka, lakini taasisi inabaki.
Leo mtu anaweza kuwa karibu sana na CHADEMA kwa sababu anaona chama kina nguvu. Kesho akabadili msimamo. Kesho kutwa akahamia chama kingine. Hiyo ni sehemu ya uhuru wake.
Lakini chama hakiwezi kubadili misingi yake kila mtu maarufu anapobadili msimamo.
Chama lazima kiwe na dira yake.
Tunataka CHADEMA iwe chama cha wanachama, sera, taasisi na misingi,
si chama kinachoendeshwa na trend za X.
MWITO WANGU KWA CHADEMA
Sasa ni wakati wa kuchukua hatua, si kubishana tu mitandaoni.
Kwanza, chama kiimarishe vikao na mifumo yake ya ndani ili maamuzi muhimu yafanywe kwa mujibu wa katiba, kanuni na misingi ya chama.
Pili, CHADEMA ijenge utamaduni wa uwajibikaji na hoja, si utamaduni wa kufuata umaarufu wa mtu. Hakuna mwanachama, kiongozi, mwanaharakati au influencer anayepaswa kuwa juu ya taasisi.
Tatu, viongozi wa chama wakumbuke kwamba nguvu yao ya msingi haitoki kwa wanaharakati, influencers wala watu maarufu mtandaoni. Nguvu ya chama inatoka kwa wanachama na wananchi wanaokipa ridhaa.
Tanganyika.Colony retweeted
Open your camera app, scan and start reading the word of God.
Tanganyika.Colony retweeted
Entire Tanzania is asking ..
#WhereIsNchimbi
Nchimbi yuko wapi?
Ki-utaratibu, na zaidi nafikiri kikatiba, ningetegemea Makamu wa Rais alie jiuluzulu, Dr. Emmanuel Nchimbi akikabidhi ofisi kwa Makamu wa sasa. Lakini mpaka sasa tokea atangaze kujiuzulu, Dr. Nchimbi hajaonekana hata uraiani. Tatizo kubwa zaidi lipo CCM na Serikali ya JMT.
CCM needs a veneer of opposition.
A controlled opposition that can dupe the public.
Without that,itapata shida.
Them forcing CDM to "maridhiano " will kill the significance of CDM/TAL.
Itakua mwisho wa relevance z/ya TAL/CDM
Oct 29 was beyond political parties or figures.
Tanganyika.Colony retweeted
Replying to @bichwaa
Kwamba CHADEMA imekufa?
Kitu pekee ambacho CHADEMA imeachieve ni kuwa movement; ukiacha TANU, hakuna chama kilichomorph na kuwa vuguvugu.
Vyama vyote vilivyoshika dola, kwa kung’oa chama tawala au kuondoa utawala wa kiimla huwa ni vyama vya harakati. Imekuwa hivyo dunia nzima
Tanganyika.Colony retweeted
LEO IMETIMIA MWEZI MMOJA TOKA PETER RICHARD MUSHI ALIPOTEKWA MAENEO YA CHINA PLAZA K/KOO.
Mpaka leo, familia na Watanzania wanaendelea kujiuliza PETER RICHARD MUSHI YUKO WAPI?
@tanpol TUNATAKA MAJIBU.
Kama Peter anashikiliwa elezeni anashikiliwa wapi?
Naomba Retweet 🙏
Tanganyika.Colony retweeted
Samia eeeh @SuluhuSamia
Hizi familia zilitamani hata walau zipate miili ya watoto wao ila haikuwa hivyo.Ulichoona cha maana wewe ni kwenda kuisomba miili hiyo baada ya kuwaua na kwenda kuwafukia kama TAKATAKA.
Ameondoka Mzee HAFIDH umeona MAUMIVU yake?
We will never forget.































